Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Bashiru akiwasiliana na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, kwa simu iliyopigwa kwenye kompyuta mpakato (Laptop) ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha CCM kuhusu Habari za Uchaguzi kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Dk. Bashiru akiangalia picha za wagombea urais kupitia CCM zilizopambwa upenuni mwa kituo hicho. Wagombea hao ni Dk. John Magufuli anayewania urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea urais Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi.
Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, Gabriel Athuman akiangalia mpangilio ulivyo ndani ya kituo hicho.
Afisa Tehama wa CCM, Magoti Wambura akimuonesha Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru, jinsi wanavyowasiliana na viongozi, wanachama na umma kupitia kwenye kompyuta mpakato wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha habari za uchaguzi.
Baadhi ya watumishi wa kituo hicho
Dk. Bashiru akiangalia kituo hicho wakati akipata maelezo kutoka kwa Afisa Tehama, Wambura (kushoto). Kulia ni Gabriel Athuman.
Afisa Tehama wa CCM, akitoa maelezo kwa Dk. Bashiru jinsi kituo hicho kitakavyopokea taarifa mbalimbaliza za uchaguzi kupitia kituo hicho.
Dk Bashiru akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ambapo alisema kuwa hivi sasa kituo hicho kitakuwa kinakusanya taarifa mbalimbali za uchaguzi kutoka kwa viongozi wa CCM, Wanachama na Umma na baada ya uchaguzi kazi yake kubwa itakuwa kukusanya Taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Dk. Bashiru akizungumza na wanahabari kuhusu kazi ya kituo hicho.
Mtumishi wa kituo hicho, Debora Kiyuga akiwa tayari ameanza kazi ya mawasiliano
Neema Mfugale akiweka mambo sawa
Zuhura Hassan akiwa kazini
Baadhi ya watumishi wakiwa kazini kituoni hapo
Social Plugin