HALMASHAURI kuu CCM mkoa wa Tanga imewapitisha kwa kauli
moja wagombea wote 245 walioomba kuwania nafasi ya udiwani katika wilaya zote
nane mkoani hapo.
Hayo yalibainishwa na Katibu
wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa katika kikao hicho cha Halmashauri kuu mkoa kilichofanyika Agosti 18 mwaka huu.
Alisema kikao hicho kiliamua kuwapitisha
wagombea wote wa udiwani walioshika nafasi ya kwanza waliopitishwa
katika kura za maoni na kwenye vikao husika vya kata wilaya kwa sababu
kiliafikiana na maoni ya vikao hivyo.
Aidha alisema mkoa wa Tanga una kata 245 zinazopatikana katika Halmshauri 11 ambapo kila kata ilitoa mgombea aliyeshinda kwa nafasi ya kwanza na kwamba katika mchakato huo hakuna aliyeshika nafasi ya pili na kupata fursa ya kuipeperusha bendera bali ni wale ambao walishinda kwenye kura za maoni ambao waliyepitishwa katika kikao hicho.
Alisema uamuzi huo umeweka rekodi ya kihistoria kwa wagombea wote waliopata nafasi ya kwanza kupitishwa katika kuwania nafasi hiyo ya udiwani na wapo waliopata nafasi ya pili na ya tatu na kuendelea lakini hawakuweza kukidhi vigezo.
Social Plugin