Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi Mkoani Dodoma limesema limejipanga kwa vizuri kwa wale wote watakaokuwa na nia ovu ya kufanya vurugu na kuhatarisha amani katika kampeni za vyama mbalimbali za siasa.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Agosti ,27,2020 jijini Dodoma Kamanda wa polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amebainisha kuwa makundi yote ya ovyo ambayo yamejiandaa kwa ajili ya kuleta vurugu yatashughulikiwa na kazi ya jeshi la polisi ni kulinda amani ya Tanzania.
“Jeshi la polisi kazi yake ni kuhakikisha kuna amani,hakutakuwepo na makundi ya Ovyo,Tanzania huwa naifananisha na mto wa maji mtulivu,mto wa maji mtulivu mara nyingi kuna kuwa na miti mikubwa ya maua mazuri imeizunguka ule mto huwezi ukaona kwa macho umetulia ndani yamto huo kuna viumbe kuna Wanyama ,wadudu,kuna mamba ,kenge wanyama wote hao wanategemea Maisha yao ndani ya mto huo yule anayekwenda kuyachezea hayo maji hakuna mnyama anayekubali kuchezewa hayo maji kenge wataenda sehemu zao na mamba sehemu zao ikimaanisha kuwa jeshi la polisi halitakaa kimya amani ya Tanzania ichezewe ”amesema.
Aidha,Kamanda Muroto amesema kuwa jeshi la Polisi litahakikisha linafuatilia kwa makini mwenendo wa kampeni na kubainisha kuwa Tanzania haina Mjomba wala shangazi nje ya nchi huku akiwataka waandishi wa Habari kutumia kalamu zao vizuri kuhakikisha hakuna Habari za uchochezi.
“Tanzania haina mjomba wala shangazi nje nchi nyingi ambazo zinatuzunguka zimekuwa zikija hapa kwa sababu zimekuwa zikipata matatizo kwa hiyo sisi kama jeshi la polisi tunahakikisha tunalinda amani na waandishi wa Habari muwe sehemu ya Watanzania kuhakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo”amesema.
Katika hatua nyingine Kamanda Muroto ametoa wito kwa watanzania kuacha watu wa kulinda nyumba pindi wanapokwenda kwenye shughuli mbalimbali ili pasitokee uhalifu wowote .
Social Plugin