Vijana jijini Dodoma wametakiwa kuacha tabia ya kuzurura ovyo mtaani bila kazi na badala yake watumie fursa kutembelea katika maeneo ya Jeshi la Kujenga Taifa [JKT]Makutupora ili waweze kujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zikiwemo kilimo,ufugaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuweza kutokomeza utegemezi.
Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma mwanzoni mwa Juma hili na mkuu wa banda la Maonesho ya Jeshi la kujenga Taifa [JKT] Makutupora Kaptain Jacob Dawson Simkoko wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema huu si wakati kwa vijana kulalamika na badala yake wanatakiwa kuchangamkia fursa zinazowazunguka ikiwemo kupata elimu ya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali kupitia Jeshi la kujenga Taifa[JKT].
“Vijana wakati huu si wa kulalalmika wanapaswa kutembelea katika maeneo ya JKT na watajifunza mbinu mbalimbali za uzalishaji mali hivyo sisi kama JKT tumekuwa mstari wa mbele kuwafundisha vijana nanma bora ya uzalishaji mali,uzalendo kwa nchi yao,kujitolea niwaase sana vijana huu si wakati wa kuzurura bila kufanya kazi”alisema.
Aidha,Kaptain Simkoko amewatoa hofu wananchi kuhusu kutembelea Jeshi la kujenga Taifa [JKT]kwani watapata fursa ya kujifunza kazi nyingi za uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi.
“Watu wengine wamekuwa wakipata hofu akisikia tu jeshi nataka niwatoe hofu watanzania Jeshi la kujenga Taifa JKT hapa utajifunza miradi mbalimbali za uzalishaji mali hakuna mabuti ni kazi kwa kwenda mbele na utapata ujuzi mbalimbali ukitembelea tu ukajionea shughuli tunazofanya utanufaika sana kwa ujenzi wa taifa letu”alibainisha.
Hirary Chale,Norbert Ndunguru na Musa Eliasy ni miongoni mwa vijana wanaonufaika na mafunzo ya Ujasiriamali katika Jeshi la kujenga Taifa,JKT Makutupora ambapo wamesema katika jeshi hilo wanajifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufugaji wa samaki,ndege aina ya kasuku ,kilimo ,ufugaji ,pamoja ufundi umeme.
“Hapa JKT Makutupora tunajikita katika shughuli mbalimbali mfano tunafuga samaki,ndege,na kilimo,tukiangalia katika suala zima la ufugaji wa samaki tumetengeneza banda la kuku juu ya maji hivyo kinyesi cha kuku hudondoka moja kwa moja majini ambacho nkula kizuri cha samaki pia huleta rangi ya kijani kwenye maji kama unavyojua samaki huwa hawapendi kuonekana kwenye maji na kuhusu jokofu la asili hili lina uwezo wa kuhifadhi mboga kwa muda wa siku 7 hadi 14 bila mazao kunyauka na limetengenezwa kwa mkaa na ni la gharama nafuu,pia tuna kasuku ambao ni kama pambo la nyumbani hivyo wamekuwa na mvuto mkubwa hapa JKT”Walisema.
Martin Sadala ni mmoja wa Walimu katika chuo cha Jeshi la kujenga Taifa [JKT]Makutupora ambapo amewaasa watu kuacha kupeleka mitaani kutengenezewa vifaa vyao zikiwemo kompyuta ili kuepuka kuibiwa na badala yake wapeleke katika maeneo rasmi ikiwemo vyuo vya ufundi huku Ratifa Nyanza ,na Khadija Juma Zayumba wakielezea umuhimu wa utengenezaji mifuko mbadala kwa urafiki wa Mazingira pamoja SUMA JKT GUARD ilivyojiimarisha katika masuala ya ulinzi.
“Martin Sadala:Mara kwa mara jamii imekuwa na desturi ya kuwapelekea mafundi wa mitaani vifaa mfano kompyuta vinapoharibika changamoto baadhi ya mafundi wa mitaani wamekuwa sio waaminifu na badala ya kutengeneza wanaiba baadhi ya vifaa muhimu na mtu anashindwa aanzie wapi kumshtaki mtu huyo njia sahihi ni kujenga mazoea ya kupeleka kifaa kwa vyuo vya ufundi ili kuepuka kuchakachuliwa”
“Ratifa Nyanza:Sisi hapa JKT tuna mradi wa utengenezaji wa bahasha ambazo ni rafiki wa Mazingira tangu serikali ikataze mifuko ya plastiki tumekuwa mstari wa mbele kuwa bega kwa began a serikali na utengenezaji wa bahasha hizi hauhitaji gharama na bahasha moja tunatengeneza kwa muda wa dakika 3 mpaka 5 tunawasihi na wengine wachangamkie fursa hii”alisema.
Ikumbukwe kuwa Jeshi la kujenga Taifa,[JKT]lilianzishwa kwa sheria ya Jeshi la kujenga Taifa[National Service Act ]ambayo ni sheria Na.16 ya mwaka 1964 ambapo sheria hiyo inatoa uwezo kwa JKT kuandikisha vijana kulitumikia jeshi hilo ambapo tangu JKT lilipoasisiwa liliandikisha vijana wa kujitolea wenye elimu ya Darasa la saba tu lakini ilipofika mwaka 1966 ilionekana kuna umuhimu kwa vijana wasomi wenye elimu zaidi ya kidato cha nne kulitumikia Jeshi hilo na sheria ilifanyiwa marekebisha na kulipa nguvu JKT kuandikisha vijana wenye taaluma zaidi ya kidato cha nne kwa mujibu wa sheria[Compulsory] na mambo muhimu yanayofundishwa ni uadilifu,umoja na mshikamano,kujitolea,uzalendo,nidhamu na kupenda kazi.