Lazaro Nyalandu, aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi, ametangaza kugombea Ubunge katika jimbo hilo kupitia CHADEMA.
Kupitia ukurasa wake Twitter Lazaro Nyalandu ameandika adhima yake hiyo ya kutaka kurudi kuwatumikia Wananchi wa Singida Kaskazini kwa nafasi ya Ubunge.
“Nitashiriki kama Mgombea katika kinyang’anyiro cha kumpata mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Jimbo la Singida Kaskazini, Uchaguzi huo utafanyika leo, Jumatatu, Agosti 10, kijijini Ilongero. Asanteni sana kwa sala na dua zenu na zaidi, kwa upendo wenu wa daima kwangu” Nyalandu
Social Plugin