Macho na masikio ya Watanzania wengine yanaelekezwa Jiji la Dodoma kutakakofanyika uteuzi wa wagombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.
Uteuzi huo unafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika ofisi zake zilizopo Ndejembi nje kidogo ya Jiji la Dodoma.
Pia, leo hiyohiyo kutafanyika uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani nchini nzima.
Uteuzi wa urais, hii ni mara ya kwanza, NEC kuendesha shughuli hiyo Dodoma baada ya kuhamia huko ikitokea jijini Dar es Salaam.
Joto la wagombea 17 waliochukua fomu zinapanda na kushuka wakisubiri kuona Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itamteua nani na kumwacha nani.
Social Plugin