Mgombea Udiwani kata ya Nyanungu Thiboche Richard akiwapungia mkono wananchi baada ya kuchukua fomu
Na Dinna Maningo,Tarime
Wanachama 34 wa Chama cha Mapinduzi (CCM)wilayani Tarime mkoani Mara wakiwemo wanawake wawili wameteuliwa kugombea Udiwani katika kata mbalimbali zilizopo Jimbo la Tarime mjini na Tarime vijijini.
Baada ya uteuzi huo zoezi la uchukuaji fomu za kugombea Udiwani zinaendelea huku shangwe,furaha maandamano vikisheheni kwenye viunga vya ofisi za vyama vya kisiasa na ofisi za wasimamizi wa uchaguzi.
Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka aliwataja wagombea hao katika jimbo la Tarime vijijini lenye kata 26 kuwa ni Thiboche Richard anaegombea kata ya Nyanungu,Thomas Nyagoryo kata ya Kibasuka,John Bosco-Regicheri,Ragita Mato-Kwihancha,William Matiko-Susuni
Wengine ni Simion Samweli kata ya Nyakonga,Marwa Marigiri kata ya Binagi,Steven Chacha-Manga,John Mhabasi-Nyarero,Siza Kiheta-Ganyange,Leonce Bartazar-Komaswa,Rashid Bogomba-Kemambo,Rhob Ghat-Kiore,Juma Matiko-Nyarukoba,Godfrey Kegoye-Matongo,Ayub Marwa-Gorong'a,Mniko Musabi-Muriba,Nashon Mchuma-Gwitiryo .
Mkaruka aliongeza kuwa Ngocho Wangwe anagombea kata ya Pemba,Samwel Mohono kata ya Nyansincha,Shadrack Mwita-Itiryo,Nyang'ondi Ndege-Bumera,Mwita Magige-Nyamwaga,Amos Sagara-Sirari,Petro Ntogoro-Mwema na Seronga Paul kutoka kata ya Mbogi.
Mkaruka alisema katika jimbo la Tarime mjini lenye kata nane wagombea ni Daniel Komote kutoka kata ya Nkende,Daud Wangwe kata ya Kitare,Chacha Machugu-Turwa,Thobias Ghat-Nyamisangura,Raymond Nelson-Mwema,Fredy Sabega-Nyandoto,Mseti Gotora-Bomani na Farida Nchagwa-Kenyamanyori.
Katibu huyo wa CCM wilaya ya Tarime aliwataka wagombea kuzingatia taratibu za chama na kufuata sheria za uchaguzi lakini pia wajikite kwenye kunadi Sera na siyo kufanya kampeni za kuchafuana na kutukanana.
Social Plugin