Mlipuko mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.Mlipuko huo umeiharibu kabisa sehemu kubwa ya bandari na majengo katika maeneo mbalimbali ya mji huo.
Maafisa wamesema zaidi ya watu 60 wamefariki na wengine zaidi ya 3,000 wamejeruhiwa, huku miili ikiwa imefukiwa katika vifusi.
Saa chache baadaye, magari ya kubebea wagonjwa yalikuwa yakiwabeba majeruhi huku helikopta za jeshi zikisaidia kuuzima moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka katika bandari hiyo.
Chanzo cha mlipuko huo, uliosababisha moto mkubwa, kupindua magari madogo na kuvunja madirisha na milango, hakikujulikana mara moja.
Social Plugin