Waziri Luhaga Mpina, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha na Kilimanjaro aliambatana na wajumbe na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya Maendeleo ya Kilimo Bw. Japhet Justine (kushoto) |
Waziri Luhaga Mpina katika ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro na Arusha
Msajili wa bodi ya nyama kutoka katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Bw.Imani Sichwale alikipongeza kiwanda cha Meat King kwa kuzalisha nyama
zilizo katika kiwango cha hali ya juu.
Na Mwandishi wetu, Arusha.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amewataka wawekezaji katika sekta ya Mifugo husasani wamiliki wa viwanda vya nyama nchini kutafuta masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.
Waziri Mpina aliyasema hayo jijini Arusha alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea viwanda vya mazao ya mifugo ambapo alisema Serikali inawaunga mkono wawekezaji katika sekta ya nyama na kushauri wafanye upanuzi wa viwanda vyao kwani baada ya janga la covid 19 biashara sasa imeanza kurudi vizuri.
“Changamkieni masoko na ziwepo products zote katika masoko ya ndani watanzani na wageni wanahitaji wazipate.”Alisisitiza.
Akiwa katika kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat king mjini Arusha Mpina aliwataka wafanye bidii katika kuhakikisha wanapata watu wanaoweza kuyafikia masoko kwa kwenda au kuwatumia mawakala hasa katika mikoa ya Mwanza, Tanga na sehemu nyingine za nchi.
Katika ziara yake kiwandani hapo Waziri Mpina, aliishauri Bank ya Maendeleo ya Kilimo TADB kuangalia uwezekano wakupanua wigo wa mikopo ili viwanda viendelee kuwepo sambamba na kuinua soko la ndani na kuimarisha mnyonyoro wa thamani wanyama na kufanya bidhaa hizo ziwe na ushindani kimataifa, kutoa ajira kwa watanzania na wafugaji wazidi kuinuliwa kiuchumi.
Akiongea katika ziara hiyo ya Waziri Mpina, Kaimu Mkurugenzi wa mikopo na biashara kutoka Bank ya Maendeleo ya Kilimo Bw. Jeremiah Muhanda, alisema Bank hiyo imeweza kuwasaidia wawekezaji kupata ,machine za kisasa, mitaji yakufanyia kazi na kuwasaidia mitaji wafugaji kupitia vikundi.
Na aliongeza kwa kusema kuwa Bank hiyo pia imewezesha kiwanda cha pembejeo za mifugo cha farm access cha mjini Arusha mkopo wa kiasi cha shilingi milioni mia nne tisini na tisa (499Milioni).
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya nyama nchini Bw. Imani Sichalwe alikipongeza kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat King kwa kuzalisha nyama yenye viwango vya juu ambapo awali ilikuwakiagizwa kutoka nje ya nchi.
Alipokuwa katika kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh Waziri Mpina alimpongeza muwekezaji huyo kwa kununua maziwa kwa wafugaji kwa bei nzuri ya shilingi mia nane themanini (880/-) kwa lita ikiwemo kuwapongeza kwa kufanya kazi nzuri ya kuzalisha lita elfu nane (8000) mpaka elfu tisa(9000)kwa siku na maziwa hayo kufika katika kila maeneo nchini.
“Serikali itaendelea kuunga mkono na kusaidia kutatua changamoto zozote na msipate vikwazo kwenye soko zuri la wafugaji wetu, ilikuweza kupata maziwa mazuri na bora...Nawasihi pia mpanue masoko kadiri mnavyoweza, nawahakikishia masoko yaliyopo yataendelea kulindwa.” Alisema.
Aidha,Waziri Mpina alielekeza bodi ya maziwa kufuatilia maziwa yanayoingizwa toka nje ya nchi kinyume na utaratibu yaondolewe na walipe kodi za serikali na nchi isiwe dampo la kuingiza bidhaa hizo kinyume nataratibu.
Alipotembelea kiwanda cha nyama cha Elia Foods Overseas ltd kilichopo Wilayani Longido,Waziri Mpina alimpongeza muwekezaji huyo kwa kufanya uamuzi wa kujenga kiwanda hicho nchini.
Hata hivyo muwekezaji huyo alimuomba Waziri Mpina kushugulikia changamoto ya kodi anayokabiliana nayo ili kuweza kuingiza vipuri toka nchi jirani ya Kenya na kuanza uzalishaji kwawakati, ambapo katika hilo Waziri Mpina alielekeza dawati la sekta binafsi la wizara yake kushughulikia changamoto hiyo mara moja ili uzalishaji katika kiwanda hicho uanze.
Ziara ya Waziri Mpina Mkoani Arusha ilihusisha kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat King, Elia Foods Overseas ltdnakiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh.
Social Plugin