MTU ALIYEDHANIWA KUWA NA UMRI MKUBWA ZAIDI DUNIANI AFARIKI DUNIA


Fredie Blom - pichani akiwa ametimiza umri wa miaka 116- alisema hauna siri ya kuishi kwake maisha marefu

Nyaraka za utambulisho za Fredie Blom zinaonesha alizaliwa tarehe 8 Mei, 1904
**
Mwanaume wa Afrika Kusini aliyedhaniwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 116.

Nyaraka za utambulisho wa Fredie Blom zinaonesha kuwa alizaliwa katika jimbo Eastern Cape mwezi Mei 1904, ingawa hilo halikuwahi kuthibitishwa na rekodi za Guinnes za dunia(Guinness World Records).

Alipokuwa kijana mwenye umri wa barehe, watu wote wa familia yake walikufa kutokana na jana la mafua -Spanish flu, mwaka 1918. Aliishi na kunusurika vita ya kwanza ya dunia pamoja na vita vya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Bwana Blom ambaye alikua mvutaji wa sigara, aliiambia BBC mwaka 2018 kwamba hakuna siri maalumu ya kuishi maisha marefu.

"Kuna kitu kimoja tu-ni mwanaume aliye juu (Mungu). Ana mamlaka yote. Sina chochote. Ninaweza kufa wakati wowote lakini bado amenishikilia,"

Bwana Blom aliishi maisha ya kufanya kazi za kawaida - ikiwemo kazi ya kilimo katika shamba na baadae katika kiwanda cha ujenzi – alistaafu akiwa na umri wa miaka zaidi ya 80.

Familia ya Bwana Blom amesema alikufa kifo cha kawaida mjini Cape Town Jumamosi.

Chanzo - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post