Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga akizungumza kwenye Studio za Radio Faraja fm 91.3 katika kipindi cha Mambo leo kinachoenda hewani kila Jumatatu hadi Ijumaa chini ya Watangazaji Josephine Charles na Irene Kishiwa.
Na Josephine Charles - Malunde 1 blog
Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wanaokata miti ovyo na kuleta uharibifu wa mazingira wametakiwa kuacha kufanya hivyo mara moja.
Akizungumza baada ya kutoa zawadi za Tisheti na miti kwa washindi wa tano waliojibu maswali kupitia kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na kituo cha Matangazo Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga kila Jumatatu hadi Ijumaa saa nne asubuhi hadi saa nane mchana chini ya Watangazaji Josephine Charles na Irene Kishiwa, Afisa Maliasili na Mazingira manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga amesema ukataji wa miti usio na tija ni hatari kwa mazingira ya Manispaa.
Amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi katika maeneo yao ya makazi na maeneo ya wazi ili kuleta mazingira mazuri na kuifanya manispaa ya Shinyanga kuwa ya kijani.
Aidha Manjerenga amewaomba wananchi kutoa taarifa wanapoona vitendo vya uharibifu wa mazingira unafanywa kwa kupiga simu idara ya maliasili na mazingira kwa namba ya simu 0765 044 948 kwa hatua zaidi.
Amewasihi washindi hao ambao ni mabalozi wa kampeni ya MTU na MTI kuhamasisha wananchi wengine katika maeneo wanayotoka kupandamiti ya matunda na kivuli kwa wingi kwa ajili ya kupata chakula na hali ya hewa safi.
Washindi hao watano ambao ni Malunguja Charles kutoka Kolandoto ambaye amechukua miti 5 ya kivuli,Athanas Silas kutoka Mwalugoye Chibe ambaye amechukua miti 3 ya kivuli na miti 3 ya matunda,Kini Dotto kutoka Katunda ambaye amechukua miti 3 ya kivuli,Mohamed Khalfan kutoka Kitangili ambaye amechukua miti 25 ya Matunda na Miti 25 ya Kivuli na Fedrick Banyikwa kutoka Ndala ambaye amechukua miti 8 ya Matunda na Miti 2 ya Kivuli kwa pamoja wameishukuru idara ya maliasili na Mazingira Manispaa kwa kuanzisha kampeni ya Mtu na Mti lengo likiwa ni kuifanya Manispaa ya Shinyanga kuwa ya kijani na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa kampeni hiyo.
Kampeni ya Mtu na Mti ilizinduliwa Rasmi 12/08/2020 katika kipindi cha Mambo leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga ambayo itakuwa endelevu baada ya kupatikana mabalozi wa kudumu ambao walipatikana kupitia kujibu maswali yaliyoulizwa katika kipindi hicho yanahusiana na mazingira,maliasili na mahusiano kati ya mtu na mti.
Leo Idadi ya miti 74 imegawiwa kwa washindi hao kwa kufuata utaratibu uliopo na kuombwa kuwa mabalozi wazuri kwa kuwatafuta watu kumi au zaidi kila mmoja ili kampeni ya Mtu na Mti izidi kuwa na mnyororo usiokatika na hatimaye kuifanya Manispaa ya Shinyanga kuwa ya Kijani na yenye mvuto.
Mmoja wa Washindi wa Tisheti waliojibu swali kwa usahihi Bw. Charles Masonga Kutoka Kolandoto akizungumza katika Kipindi Cha Mambo leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga akiwa amevaa tisheti yake yenye Nembo ya Mtu na Mti.
Mmoja wa Washindi wa Tisheti waliojibu swali kwa usahihi Bw
Kini Dotto Kutoka Katunda akizungumza katika Kipindi Cha Mambo leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga akiwa amevalia tisheti yake yenye Nembo ya Mtu na Mti
Wa kwanza kulia ni mmoja wa Watangazaji wa Kipindi hicho Bi. Irene Kishiwa.
Kini Dotto Kutoka Katunda akizungumza katika Kipindi Cha Mambo leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga akiwa amevalia tisheti yake yenye Nembo ya Mtu na Mti
Wa kwanza kulia ni mmoja wa Watangazaji wa Kipindi hicho Bi. Irene Kishiwa.
Kutoka Kushoto ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga, wanaofuatia ni baadhi ya Washindi wa Tisheti Bw. Kini Dotto,Athanas Silas na Fedrick Banyikwa.
Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga akizungumza kwenye Studio za Radio Faraja fm 91.3 katika kipindi cha Mambo leo kinachoenda hewani kila Jumatatu hadi Ijumaa chini ya Watangazaji Josephine Charles na Irene Kishiwa.
Mmoja wa Washindi wa Tisheti waliojibu swali kwa usahihi Bwana.Fedrick Banyikwa Kutoka Ndala akizungumza katika Kipindi Cha Mambo leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga akiwa amevalia tisheti yake yenye Nembo ya Mtu na Mti.
Mmoja wa washindi wa Tisheti Bw. Athanas Silas akielezea namna atakavyokuwa Balozi mzuri wa Kampeni ya Mtu na Mti katika Manispaa ya Shinyanga mara baada ya kuulizwa na Mtangazaji Josephine Charles aliyevaa Headphone katika studio za Radio Faraja fm - kipindi cha Mambo leo.
Mmoja wa Washindi wa Tisheti waliojibu swali kwa usahihi Bwana.Athanas Silas Kutoka Mwalugoye Chibe akizungumza katika Kipindi Cha Mambo leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga akiwa amevalia tisheti yake yenye Nembo ya Mtu na Mti.
Mmoja wa Washindi wa Tisheti waliojibu swali kwa usahihi Bw. Fedrick Banyikwa Kutoka Ndala akizungumza katika Kipindi Cha Mambo leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga akiwa amevalia tisheti yake yenye Nembo ya Mtu na Mti.
Mmoja wa washindi wa Tisheti Bw. Kini Dotto akielezea namna atakavyokuwa Balozi mzuri wa Kampeni ya Mtu na Mti katika Manispaa ya Shinyanga mara baada ya kuulizwa na Mtangazaji Josephine Charles aliyevaa Headphone katika studio za Radio Faraja fm - kipindi cha Mambo leo.
Waliosimama kutoka Kushoto ni Mtangazaji wa Kipindi cha MAMBO LEO Irene Kishiwa,Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga,Washindi wa Tisheti Kini Dotto,Athanas Silas,Mohamed Khalfani na Waliochuchumaa kutoka Kulia ni Mtangazaji wa Kipindi cha MAMBO LEO Josephine Charles,washindi wa Tisheti Fedrick Banyikwa na Malunguja Charles,wakiwa katika picha pamoja katika Viwanja vya Radio faraja fm 91.3 Shinyanga mara baada ya kufanyika kwa kipindi.
Picha zote na Edward Mangu.
Social Plugin