Mgombea Ubunge Jimbo lá Muheza Hamis Mwinjuma alimaarufu Mwana FA kulia
akipokea fomu za kuwania Ubunge Jimbo lá Muheza kutoka kwa msimamizi wa
Uchaguzi Katika Jimbo hilo Nassib Mbaga |
Mgombea Ubunge Jimbo lá Muheza Hamis Mwinjuma alimaarufu Mwana FA |
Mgombea Ubunge Jimbo lá Muheza Hamis Mwinjuma alimaarufu Mwana FA katikati akiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo wakikimbia kwenye maeneo mbalimbali wilayani Muheza kuelekea ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza kuchukua fomu
Mgombea Ubunge Jimbo lá Muheza Hamis Mwinjuma alimaarufu Mwana FA katikati akiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo wakiiingia kwenye ofisi za CCM wilaya ya Muheza baada ya kutoka kwenye ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza kuchukua fomu
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Muheza akizungumza wakati wa halfa hiyo
KATIBU wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo akizungumza wakati wa mapokezi ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo
MGOMBEA bunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufika ofisi za CCM wilaya ya Muheza leo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo
MAPOKEZI ya Mgombea Ubunge Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi
Mwinjuma maarufu MwanaFA yamevunja rekodi katika wilaya ya Muheza mkoani
Tanga huku akihaidi kupigania mahitaji ya wasanii pindi akichaguliwa
kuwa mbunge wa Jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
MwanaFA pia alishangazwa na mapokezi aliyopata kutoka kwa
wananchi wa wilaya ya Muheza hali ambayo ilimtoa machozi na kusimamisha
huduma mjini Muheza kwa muda wa saa 2 kuanzia muda wa saa 5:00 asubuhi
hadi saa 7:00 kamili mchana.
Msafara wa kwenda kumpokea MwanaFA kutoka kijijini kwao
Kwemhanya kata ya Mtindiro ulianza kuondoka Muheza Mjini majira ya saa
4:30 asubuhi kuelekea katika kijiji cha Kibanda umbali wa kilometa 7
kutoka Muheza Mjini.
Majira ya saa 5:00 asubuhi MwanaFA aliwasili katika kijiji
cha Kibanda katika barabara kuu ya Tanga-Segera ambapo alikuwa umati
mkubwa wa watu ukimsubiri wakiwa kwa miguu,magari na bodaboda jambo
ambalo lilimfanya ataharuki na kutoa machozi.
Msafara ulianza kuelekea kuliekea hadi katika ofisi za
Makao Makuu ya CCM wilayani Muheza 11:43 akisindikizwa katika gari la
wazi huku akiifuatuliza nyimbo zake ambapo alikwenda kusaini katika
kitabu cha wageni baada ya hapo alitembea kwa miguu kwa maandamano
kupitia barabara ya soko kuu la mbogamboga na matunda-Amtco -stendi
kuu-hadi Bomani katika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Muheza.
Saa 6:17 Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Muheza Nasibu Mbaga
alikabidhi fomu nne za NEC na kupewa maelekezo ya namna ya kuzijaza
ambapo alikuwa ni mgombea wa saba huku akitanguliwa na wagombea wengine
wa ubunge wa jimbo hilo kupitia vyama vya CUF,ACT-Wazalendo,NCCR- Mageuzi,UDP,na AAFP.
Saa 6:19 alitia saini katika kitabu cha Wageni cha NEC na
kuondoka kuelekea tena katika ofisi za CCM Muheza ambapo alifika majira
ya saa 6:45 ambapo aliongea na wananchi.
Saa 7:00 alimaliza kuongea na majira ya saa 7:31 alifanyiwa tambiko za kimila za kabila la kibondei.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuchukua fomu za NEC alisema kuwa amesukumwa kuja kugombea jimbo la
Muheza kutokana na kero mbili kuu ambazo kwa muda mrefu limekuwa ni
tatizo sugu kwa wananchi wa Muheza ambazo ni changamoto ya maji na
barabara ya Muheza- Amani yenye urefu wa kilometa 35 ambayo ipo katika
kiwango cha changarawe ambapo katika kipindi cha mvua huwa haipitiki.
"Watu wote tunajua kuwa Muheza kuna tatizo la maji,kwa mara
ya kwanza nilikutana na mama mmoja akinionesha kichwa chake
kimonyonyoka nywele akaniambia ni kwasababu ya kubeba maji,na pili
wenzetu wa Amani wanapata tabu sana kwenye kipindi cha mvua barabara
haipitiki,"alisema.
Kuhusu maslahi ya wasanii amesema "nitahakikisha ninatetea
mahitaji ya wasanii kwa ujumla nikiwa bungeni kutokana nitakuwa mmoja
kati ya watunga sheria,hivyo wasanii sitawaangusha"
Saa 8:00 aliondoka Muheza ambapo aliongozana na bondia wa
ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo ambaye alipokelewa katika mji wa Pongwe
akitokea Dar es salaam baada ya pambano lake la ngumi la Kimataifa hivi
karibuni jijini Dar.
Social Plugin