Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Bodi ya Magavana wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, MWEKA wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa hafla hiyo iliyofanyika Chuoni hapo Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu akimkabidhi begi yenye vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Prof. Faustine Bee wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jana katika Chuo hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu
ameamuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa kitalu
cha Uwindaji wa Kitalii kwa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka
ili kitumike kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosomea
masomo ya Uwindaji Bingwa (Professional Hunters)
Ametoa agizo hilo leo
wakati akizindua Bodi ya Magavana ya Chuo cha Usimamizi wa
Wanyamapori, Mweka kilichopo katika wilaya ya Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Mhe. Kanyasu amesema Kitalu hicho Uwindaji wa kitalii kitakisaidia Chuo hicho kuzalisha
wataalamu wenye sifa.
Amesema kwa sasa Mabingwa wa Uwindaji wa Kitalii wanaofanya kazi hiyo
hapa nchini ni raia wa kigeni na baadhi ya Wazawa waliopo ni Wazee.
Amesema kitalu hicho kitachochea kupata Wataalamu wa kutosha ili kuweza kukabiliana na uhaba wa Wataalamu wa fani hiyo.
Aidha,
Mhe. Kanyasu amesema
Chuo hicho kitasaidia kukabiliana na Wafugaji wanaoingiza vitalu vya
uwindaji wa kitalii kwa vile vitalu vingi bado vipo wazi hali
inayopelekea Wafugaji wengi kuingiza mifugo hivyo
Pia,
Amesema Kitalu hicho hakitasaidia Wahitimu pekee kufanya mafunzo kwa
vitendo bali itasaidia Wanyamapori kuwa salama kwa sababu Chuo hicho
kitakuwa na jukumu la kupambana na tatizo la ujangili.
Awali, Mkuu wa Chuo hicho, Prof.
Jaffari Kidegesho amesema kwa sasa Wanafunzi wa Chuo hicho wamekosa maeneo
ya kufanyia mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya uwindaji wa kitalii.
Amesema
mwanzo Chuo hicho kilikuwa kikiyatumia Mapori ya Akiba kwa ajili ya
mafunzo hayo ila kwa sasa mapori hayo yamepandishwa hadhi na
kuwa Hifadhi za Taifa hivyo katika Hifadhi hizo hakuna shughuli za
kibindamu zinazoruhusiwa kufanyika kwa mujibu wa sheria.
Naye,
Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori, Mweka, Prof. Jaffari Kidegesho amesema kitalu hicho kitasaidia kufanya mafunzo kwa
vitendo na hivyo kutasaidia kuwaandaa wahitimu wenye sifa kulingana na mahitaji ya
soko
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki amekitaka Chuo hicho kuboresha mtaala wa
mafunzo hayo ili kuzalisha Wataalamu wataoweza kujibu changamoto za
soko.
Kwa upande wake Mkuu wa
wilaya ya Kilimanjaro, Alhaji Rajabu Kundya amesema suala la uhifadhi
na utalii limekuwa na mchango mkubwa sana kwa uchumi wa Taifa hali
iliyopelekea Tanzania kuwa na Uchumi.
Amesema
shughuli hizo wanazichukulia kwa uzito mkubwa na wanakithamini sana
Chuo hicho kwa mchango mkubwa wa kuzalisha Wasomi wenye weledi.
Itakumbukwa
kuwa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka ndo chuo pekee nchini
kinachotoa mafunzo ya Uwindaji Bingwa wa Kitalii (PH)
Social Plugin