Ndege ya Shirika la Air India iliyokuwa na abiria karibu 200 imeanguka katika uwanja wa ndege wa Calicut .
Ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Dubai, ilianguka wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa jimbo la Kusini mwa India, Kerala.
Shughuli za uokoaji zinaendelea, huku huduma za dharura zikiwa zinaendelea uwanjani hapo.
Bado haijafahamika kama kuna madhara yoyote yaliyotokea. Picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zimeonesha ndege hiyo iliwa imevunjika vipande viwili.
Tukio hilo limetokea mwendo wa saa moja kwa saa za eneo hilo kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha
Kumekuwepo na mafuriko na maporomoko ya udongo, wakati huu wa kipindi cha monsoon.
Credit:BBC
Credit:BBC
Social Plugin