Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) leo Agosti 26, imezungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo uchaguzi, ambapo kubwa zaidi wametoa rai kwa vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa weledi zaidi katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Wilson Mahera amesema, hadi kufikia 6:32 mchana, tume hiyo ilikuwa haijapokea pingamizi lolote la nafasi ya urais. Mwisho wa kuweka pingamizi ni saa 10 jioni.
“Agosti 25,2020 tume ilikamilisha uteuzi wagombea urais na makamu, ubunge na udiwani, hatujatoa taarifa yoyote juu ya zoezi hili, tayari vyombo vya habari kadhaa vinaaza kutoa matokeo ya uteuzi huu, hii ni kinyume na sheria.
”Unapotangaza mtu amepita bila kupingwa hiyo inaweza pelekea uvunjifu wa amani pale mtu anapowekewa mapingamizi, isionekane ameshinda. Mimi mwenyewe mkurugenzi wa uchaguzi sijapata majina hayo rasmi.
”Kumekuwepo na dhana ambayo wanadhani watu wanakatwa, suala la uteuzi huwezi kukata mtu kwa matakwa yako, sababu tume inafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, tumeweka masharti ya uteuzi kwa urais wa Tanzania, ubunge na udiwani.
“Unapowekea mtu pingamizi au ukiona hakuteuliwa maana yake hajatekeleza masharti, mtu akitoa maneno nje ya masharti hatafanikiwa sababau huyu akitaka rufaa atashinda. Tume inafanya kazi kwa uwazi na uhuru,” amesema Dkt. Mahera.
Social Plugin