Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inafuatilia zoezi la kuchukua fomu za uteuzi na kubaini kuwa kuna changamoto ambazo zimejitokeza kutokana na vyama vya siasa kutokujipanga na kuweka utaratibu mzuri wa Wagombea wao kuchukua fomu za Uteuzi.
Tume imesema kutokana na hilo watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao wamejitokeza na kwenda kuchukua fomu za uteuzi za kugombea Ubunge au Udiwani bila ridhaa ya vyama husika na kupelekea walioteuliwa kushindwa kuchukua fomu.
Kwa mujibu wa Tume hiyo Majimbo yaliyoathirika ni Kibamba, Mbagala, Kilombero, na Kigamboni.
Hivyo, Tume imetoa nafasi kwa vyama vya siasa kuwatambulisha Wagombea wao kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ndani ya siku 2 kuanzia Agosti 20, 2020 kwa majimbo na Kata zilizo na changamoto
Social Plugin