NIDA YAFUNGA MITAMBO MIPYA KUMALIZA TATIZO LA VITAMBULISHO

Na Samirah Yusuph

Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA imefunga mitambo miwili ya kisasa kwa ajiri ya kukamilisha uzalishaji wa  vitambulisho uliokwama.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa mamlaka hiyo Geofrey Tengeneza alisema, hapo awali mitambo ilichakaa na kufikia hatua ya kuzalisha vitambulisho 200 hadi 500 kwa siku hali iliyofanya kuwa na mrundikano wa vitambulisho ambavyo vinasubiri kutengenezwa.

"Katika kituo chetu kikuu cha uzalishaji mitambo ilichoka na ikawa inazalisha kwa kiwango kidogo na hiyo ilitufanya kishindwa kufikia malengo yetu ya kutoa vitambulisho kwa wakati," alisema.

Aliongeza kuwa, kwa sasa wamejipanga kumaliza tatizo hilo kwa sababu wamefunga mitambo mikubwa ambayo kwa saa moja itazalisha vitambulisho 4500. na kwa siku vitazalishwa 144,000.

"Mitambo tuliyoifunga kwa sasa tunaamini ndani ya muda mchache tutamaliza zoezi la kutoa vitambulisho, niwaombe wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi ili wapate vitbulisho na ambao tayari wana namba waende ofisi za mtaa wakachukue vitambulisho.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kutunza vitambulisho vyao, kwani umapo poteza atakibidi kuweza kulipia kiasi cha Sh 20000 kwa ajili ya kitambulisho kingine.

"Watu wengi wanakuwa hawapo makini katika kutunza vitambulisho hivi niwatake wananchi kuvitunza kwa dhati kuepuka usumbufu pindi kipoteapo," alisema.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post