Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli ameahidi kufanya upanuzi wa barabara na kujenga vibanda vya Wajasiriamali katika eneo la Dumila, Wilaya ya Mvomelo Mkoani Morogoro.Pichani ni Rais Magufuli akila Mhindi wa Kuchoma katika eneo la Dumila Darajani wakati aliposimama kuzungumza na wafanyabiashara hao wadogowadogo akiwa njiani kuelekea Dodoma.(Picha IKULU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Mhindi wa Kuchoma kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.
Wafanyabiashara wa Dumila Darajani
wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli kusimama katika eneo hilo wakati akiwa njiani kuelekea
Dodoma.
Social Plugin