Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameibuka ndani ya Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo.
Mkutano huo unafanyika leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Lissu aliingia ukumbini wakati Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo akijiandaa kutoa hotuba kwa wajumbe wa mkutano huo.
Kabla hajaanza, Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, akaingia ukumbini akiwa ameambatana na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar.
Kabla hajakaa katika nafasi iliyokuwa imeandaliwa, Zitto alimwita Lissu na Bernard Membe, Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo wapande jukwaani hali iliyoibua shangwe zaidi.
Membe anatarajiwa kuteuliwa na mkutano huo kuwa mgombea urais
Social Plugin