Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichofanyika jijini Dodoma .
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo zaidi kwenye kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Masoko na Uzalishaji Dkt. Felix Nandonde,akitoa taarifa kwenye kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichoongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel kilichofanyika jijini Dodoma.
Meneja wa kituo cha huduma za forodha TRA Bw.Sume Kunambi akitoa maoni kwa wadau waliohudhuria kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichoongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel kilichofanyika jijini Dodoma
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,Josephine Mhando akizungumza wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichoongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel kilichofanyika jijini Dodoma.
Meneja Masoko na Maendeleo ya Biashara Bw.Jeremiah Kilato akichangia mada wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichoongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mradi Tanzania Milk Processing Project (TMPP),Mark Tsoxo akitoa mchango wake kwenye kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichoongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel kilichofanyika jijini Dodoma
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kumaliza kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kilichofanyika jijini Dodoma
.............................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel ameiagiza Bodi ya Nyama nchini kuandaa mpango mkakati wa biashara ya uuzaji wa nyama ya kuku kwa kutumia mizani ili kuondokana na utaratibu uliozoeleka kwa muda mrefu wa kufanya biashara hiyo kwa kukadiria uzito.
Kauli hiyo ametoa jijini Dodoma wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na mashirika pamoja na wadau mbalimbali katika sekta ya mifugo kwa mwaka wa 2019/2020.
Prof.Gabriel amesema kuwa umefika wakati sasa biashara ya uuzaji wa nyama ya kuku kufanyika kwa kutumia mizani kupima kilo kama inavyofanywa kwa mazao mengine ya Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo.
Aidha aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano lengo lake ni kuona mazingira wezeshi yanatengenezwa ili waliowekeza waweze kufanya kazi yao kwa utaratibu mzuri na Serikali iweze kukusanya mapato yake halali.
"Lengo la Wizara ni kuhakikisha kwamba wadau mliopo katika sekta Binafsi mnajengewa mazingira mazuri ya kufanya kazi zenu vizuri kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni tukitegemea kwamba hatutahitajika kutumia nguvu nyingi ili mtii sheria, na hilo ndio lengo la Serikali," amesema Prof. Gabriel
Hata hivyo Prof. Gabriel amewaeleza wadau kuwa katika sekta binafsi kila kitu ni fursa hivyo ni lazima wawe wabunifu ili kuboresha biashara zao.
"Ndani ya Wizara kuna dawati la Sekta Binafsi pale ndio sehemu tunaendesha mipango ya biashara iweje na tunafanya bure, hivyo litumieni" amesisitiza Prof Gabriel
"Nyama ya kuku kuuzwa kwa kilo ni jambo zuri sana maana nyama zingine wanauza kwa kilo hivyo itakuwa vyema bodi ya nyama ikashughulikia jambo hilo ili nyama ya kuku nayo ikawa inauzwa kwa kilo," aliongeza
Aidha, Prof. Gabriel amewataka wale wazalishaji feki wa kuku na kwa chochote kile wanachokifanya wakae chonjo kwa sababu Serikali haina mzaha na yeyote anayejihusisha na uvunjifu wa sheria , taratibu na kanuni huku akisisitiza kuwa wataendesha operesheni kuhakikidha kwamba wanawapata wale wote watakaokwenda kinyume na aagizo hilo.
Kuhusu tasnia ya Maziwa, Prof. Gabriel ametoa wito kwa wafugaji kuhakikisha kuwa wanatoa bidhaa bora kwa kuzingatia kanuni za ufugaji ili watoe maziwa bora yatakayouzika vizuri sokoni.
Prof. Gabriel amewatia moyo wadau hao kwa kuwaeleza kuwa pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo hawana sababu yoyote ya kukata tamaa, Serikali ipo nao kuhakikisha kwamba sekta hiyo ya mifugo inazidi kukua kwa asilimia tano na inachangia pato la taifa kwa asilimia 7.5.
Pia, amewataka wadau hao kuendelea kushirikiana na Serikali kwani kwa kufanya hivyo mchango wao katika pato la taifa utazidi kuongezeka huku akiwakumbusha kuwa ni lazma wajue kwamba wako kwenye biashara na kazi ya Serikali ni kuwajengea mazingira wezeshi.
Katika hatua nyingine, Prof. Gabriel ametoa rai kwa vijana na kuwahimiza kuchangamkia fursa zilizopo, hususani kwenye sekta ya Mifugo ili waweze kujikwamua kimaisha kwani fursa ziko nyingi na mitaji ipo kupitia dawati la sekta binafsi.