Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais John Pombe Magufuli, amependekeza kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 za chama hicho, zizinduliwe jijini Dodoma.
Dk. Magufuli ambaye ni Rais wa Tanzania ametoa pendekezo hilo leo Alhamisi tarehe 6 Agosti 2020 makao makuu ya chama hicho, mara baada ya kutoka Ofisi za NEC jijini Dodoma kuchukua fomu za kuwania Urais wan chi hiyo.
Akizungumza na mamia ya wanachama waliojitokeza ofisini hapo, Rais Magufuli amesema, “Ninawaomba viongozi wenzangu tukizindua kampeni tuzianzie hapa Dodoma, kwa sababu ndiyo Makao Makuu ya nchi, ninawashukuru kwa mapokezi haya mazuri”
Hata hivyo, Rais Magufuli, hakupendekeza tarehe ya uzinduzi huo wa kampeni.
Ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaonyesha kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, zitaanza 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.
Amesema, chama hicho kimeandaa Ilani ya Uchaguzi ya CCM nzuri na yenye mambo mengi yenye tija kwa Watanzania wote bila kujali kidini, kabila au itikadi za kisiasa.
Social Plugin