Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUONGEZA SIKU MBILI ZA KUFANYIKA MAONESHO YA KILIMO NANE NANE


Serikali imetangaza kuongeza muda wa siku mbili za kufanyika kwa maonesho ya Kilimo ya Nanenane kote nchini ikiwa na lengo la kuwezesha wakulima, wafugaji , wavuvi  na wananchi wengi zaidi kufika kwenye viwanja vya maonesho kujifunza kanuni bora za uzalishaji mazao, teknolojia mpya pamoja na fursa za masoko ya mazao yao. 


Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet N.Hasunga leo alipongea na waandishi wa habari kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane Nyakabindi mkoani Simiyu. 


“Muda wa maonesho ya Nanenane ni siku nane.Hata hivyo, mwaka huu sherehe zimechelewa kuanza baadhi ya kanda. Kulingana na mahitaji ya sherehe hizi kitaifa kilele kitakuwa siku ya tarehe 08 Agosti, 2020. Hivyo,tumeamua kuongeza siku mbili ya Jumapili na Jumatatu ili wananchi ambao hawakupata nafasi wapate kushiriki “ alisema Waziri Hasunga 


Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane mwaka huu inasema “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”
Imetolewa na ;

Revocatus A. Kassimba
Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano Serikalini.
WIZARA YA KILIMO
 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com