Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema huenda kusiwepo tiba ya haraka ya Ugonjwa wa Covid-19 na kwamba itachukua muda mrefu kabla hali kurudi kuwa ya kawaida katika baadhi ya maeneo mbalimbali duniani.
Takwimu zinaonesha kuwa watu miliomi 18 kote duniani wameambukizwa virusi vinavyosababisha homa ya mapafu ‘Corona’ na karibu laki 7 wamefariki dunia.
Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amezitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kiafya za kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.
Naye Mkuu wa Masuala ya Dharura katika Shirika hilo, Mike Ryan amesema nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi zinastahili kujiandaa kwa mapambano makubwa.