Rais Donald Trump wa Marekani amesema jana kwamba anapanga kuupiga marufuku mtandao wa kijamii wa Tik Tok, saa kadhaa baada ya minong'ono kusambaa kuhusu uwezekano wa serikali yake kuchukua hatua dhidi ya Tik Tok.
Trump alinukuliwa na waandishi wa habari kwenye ndege ya rais ya Air Force One akisema wataizuia App hiyo nchini Marekani.
Trump alikuwa anarejea Ikulu ya White House akitokea Florida.
Aliongeza kuwa anaweza kutumia mamlaka ya dharura ya kiuchumi ama amri ya rais kuizuia Tik Tok na kusisitiza kwamba anayo mamlaka na amri hiyo itasainiwa leo.
Mapema wiki hii serikali ya Trump ilitaka App hiyo kupitiwa upya na tume ya uwekezaji wa nje nchini humo, CFIUS, huku kukiwa na wasiwasi kwamba China huenda inaitumia kuichunguza Marekani.
Social Plugin