Chama cha Republican nchini Marekani jana kimemuidhinisha Donald Trump kuwa mgombea wake wa kiti cha urais katika uchaguzi wa Novemba ambao kiongozi huyo atawania muhula wa pili.
Tangazo rasmi la kuidhinishwa kwa Trump limetolewa wakati wa siku ya kwanza ya mkutano mkuu wa taifa wa chama cha Republican unaofanyika katika jimbo la Carolina Kaskazini.
Akihutubia mkutano huo baada ya kuteueliwa kuwa mgombea, Trump amesema iwapo hatochaguliwa kwa kipindi cha pili uchumi na ustawi wa nchi hiyo utakabiliwa na hali mbaya.
Pia aliitumia hotuba yake kukishambulia chama hasimu cha Democratic kuwa kinapanga kutumia wasiwasi wa janga la virusi vya coorna kufanya udanganyifu na wizi wa kura katika uchaguzi wa Novemba.
Mwanasiasa huyo anakabiliwa na hali ngumu katika uchaguzi unaokuja kutokana na jinsi anavyoshughulia janga la virusi vya corona ambalo limesababsiha vifo vya maelfu ya watu, kuharibu uchumi na kulemaza shughuli za uzalishaji.
Credit:DW
Social Plugin