Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia shilingi bilioni 331.7 kukamilisha uchaguzi mkuu utakofanyika Oktoba 28, 2020, ambapo fedha hizo zitatolewa na serikali.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage amesema fedha hizo zitatolewa kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina kwa kuzingatia kifungu cha 122 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi , hatua iliyopongezwa kwa serikali kugharamia uchaguzi huo.
Jaji Kaijage ameongeza kuwa jumla ya wapiga kura milioni 29.2 wamejiandikisha kupiga kura za madiwani, wawakilishi, wabunge na Rais.
Amesema kutokana na idadi hiyo ya wapiga kura, kutakuwa na vituo 80,155 vya kupigia kura na kila kituo kimoja kitahudumia wapiga kura wasiozidi 500.
Social Plugin