Vijana Wa Jeshi La Akiba Moshi DC "Kupigwa Msasa" Na Vyombo Vya Usalama

Na Dixon Busagaga ,Moshi
IDARA za serikali zikiwemo Jeshi la Polisi ,Usalama wa Taifa ,Taasisi ya kuzia na kupambana na Rushwa nchni (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la zima moto na uokoaji zimetajwa kuhusika katika mafunzo kwa kundi la 50 la vijana wanaojiunga na jeshi la akiba katika wilaya ya Moshi.

Uzalendo ,Uzalendo,Uzalendo ni maneno ambayo yamekuwa yakihubiriwa kwa kundi la vijana yakilenga kundi hili kujitoa kwa ajili ya nchi yao kama inavyoonekana kwa vijana hawa waliojitolea kujiunga na jeshi la akiba.

Vijana 111 kutoka tarafa ya Kibosho katika wilaya ya Moshi miongoni mwao 97 wakiwa ni wanaume na 14 wakiwa ni wanawake wameanza mafunzo yatakayodumu kwa zaidi ya majuma 18 kama anavyoeleleza Kepteni Hansi Mwakanyamale ,kiongozi wa mafunzo hayo.

“Vijana waliojitolea kujiunga na jeshi la akiba ,mafunzo yataendeshwa kwa majuma 18,masomo watakayo jifunza ni nadharia na vitendo yakiwemo masomo ya Kwata,Uraia ,Usomaji wa ramani ,Mbinu za kivita ,ujanja wa porini,huduma za kwanza .silaha ,sharia za jeshi ,muundo wa jeshi ,utimamu wa mwili ,uhandisi wa medani ,mapigano ya singe ,vita msituni ,uzalendo na usalama wa raia”alisema Kepteni Mwakanyamale.

Alisema mmani ya jeshi la akiba wilaya ya Moshi ni kuhakikisha kwamba mkaazi wa wilaya hiyo atakayehudhuria na kufaulu mafunzo hayo anakua ni tegemeo la nchi na kiusalama kwa watanzania wote na kwamba anakua ni tegemeo la watanzania wengine ambao hawajapata nafasi ya kufanya mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo Katibu tawala msaidizi Nathanieli Mshana alisema vijan hao wameonesha uzalendo kwa nchi yao na kwamba mafunzo haya yatasaidia kuwajengea ukakamavu na ujasili mkubwa miongoni mwa vijana wengine .

Hili ni kundi la 50 la vijana walioamua kujiunga na mafunzo katika jeshi la akiba katika wilaya ya Moshi ,mafunzo ambayo yamekuwa msaada hasa kwa vijana kwa kuwajengea uzalendo na ukakamavu.

MWISHO


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post