Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akibeba tofali na kupeleka katika
jengo jipya linaloendelea kujengwa katika kwanda cha ngozi cha
karanga Mkoani kilimanjaro.
Wafugaji katika kijiji cha Miti Mirefu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kulipa deni la kiasi cha Shilingi Milioni kumi na tisa, wanalodaiwa na Serikali ikiwa ni faini iliyotokana na kukiuka mkataba wa kuingiza mifugo kwa ajili ya malisho katika ranchi ya West Kilimanjaro, inayomilikiwa na Shirika la Ranchi zaTaifa (NARCO).
Hatua hiyo imechukuliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipofanya ziara katika Ranchi hiyo na kusikiliza changamoto zinazowakabili wafugaji katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuwa na eneo dogo la kulishia mifugo,josho nazahanati kwa ajili ya matibabu yao.
Baada ya kuwasilisha changamoto ya eneo la kulishia mifugo ndipo Waziri Mpina alipoongea kwamsisitizo kuwa“ Mmekiuka mkataba mlioingia na Serikali baada ya kupewa kibali cha kulishia mifugo katika ranchi ya Taifa,deni la shilingimilioni 19 lilipwe ndani ya siku kumi na tano (15) na lisipolipwa mkataba uvunjwe, hizini maliza Serikali hatuwezi kuziendesha kwa namna ambavyo kila mtu anataka.” Alisema.
Akitoleaufafanuziswalala josho, Waziri Mpina alisema hakuna maelezo ya kutosha kwa nini josho la zamani halijakarabatiwa na kuagiza Taasisi ya Tafiti za Mifugo (Tariri) kukarabati josho hilo kwa siku kumi na tano na kusema kuwa baada ya zoezi hilo serikali itawaletea wafugaji dawa za ruzuku za kuogeshea mifugoyao.
Kwa upande wa Changamoto ya zahanati, Mpina ameelekeza Shirika la Ranchi zaTaifa (NARCO) kukarabati jengo moja chakavu ili liweze kutumika kama zahanati katika kijiji hicho na Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri kuleta wataalam na madawa tiba.
Waziri Mpina alisema ili kuweza kuwasiadia wafugaji hao kupata suluhisho la kudumu la eneo la malisho upatikane muda wa kutosha wa kulifanyia kazi swala hilo ili liweze kupatikana eneo la uhakika na la kudumu .
“Ni kazi ya Serikali kuhakikisha Changamoto hizo za wafugaji zinatatuliwa kwa wakati kama tulivyofanikisha kupunguza gharama za chanjo za mifugo kutoka shilingi elfu moja (1,000/-) mpakaelfutano (5,000/-) hapoawali mpaka shilingi miatano (500) kwasasa, sambamba nakushusha gharama za kuogesha mifugo ambazo kwa sasa kuosha ngombe mmoja ni shilingi hamsini (50) na mbuzi na kondoo ni shilingi ishirini (20), kwa hivyo hiyo changamoto ya mipaka itashughuliwa na wataalam kutoka wizara husika.” Alisema.
Awali, Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha kuchataka ngozi kinachomilikiwa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mifuko ya hifadhi ya jamii ya (PSSSF )kilichopo Karanga mjini Moshi na kujionea vifaa vya uzalishaji vilivyopo katika kiwanda hicho na namna ujenzi unaendelea na kuwataka kumaliza shughuli hizo za ujenzi kwa wakati ili kuanza uchakataji na uzalishaji utakaoliletea Taifa tija kwa kuuza bidhaa zitokanazo na ngozi nje ya nchi na kongeza pato la Taifa.
“Tunawauzia ngozi za ng’ombe wetu wanakuja na bidhaa kamaviatu,mapochi na mikanda na kutuuzia bei ghali wakati sisi wenyewe tuna uwezo wakuzalisha bidhaa hizo hapa nyumbani na kuwauzia wao,wakati umefika sasa wa sisi kutumia zao hili la mifugo kuliongezea pato Taifa.” Alisema.
Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara kutoka Bank yakilimo (TADB) Bw. Jeremiah Mhada amesema kwa sasa bank hiyo inafanya kazi kwa karibu na shirika la Ranchi zaTaifa NARCO hii ni katika kuhakikisha kwamba ranchi hizo zinaweza kujiendesha kibiashara na tayari wameshapokea maombi ya mkopo kutoka ranchi ya Kongwa Dodoma na wanayafanyia kazi.
Ziara hiyo ya Waziri Mpina Mkoani Kilimanjaro ni matokeo ya utekelezaji wa majukumu yake katika kuendelea kuimarisha na kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi nchini.