WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUTOVURUGA AMANI YA NCHI

Na Samirah Yusuph Simiyu

Wasimamizi wa uchaguzi wameaswa kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi na kutokujihusisha na vitendo viovu ambavyo vitaashiria kuharibu uchaguzi na kuvuruga amani ya nchi.

Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa uchaguzi mkoa Simiyu Saimon Maganga, alipokuwa akifungua mafunzo ya kuwaandaa wasimamizi wa uchaguzi mjini bariadi.

Maganga alisema kuwa wameaminiwa kubeba jukumu hilo zito kwa hiyo na wao wajiaminishe kwa kufanya kazi kwa utii bila kukiuka kanuni na muongozo ambao umetolewa na tume ya uchaguzi.

" Tunaimani na nyinyi na tunaamini baada ya uchaguzi tutakuwa na amani yetu, msitumike katika kuharibu uchaguzi mkafanye kile kilichokusudiwa na tume yetu kwa uaminifu na uadilifu mkubwa," alisema maganga.

Wakizungumza kuhusu mafunzo wanayo yapata baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi wamesema mafunzo hayo yanawajengea uelewa mpana kuhusu uchaguzi na kuahidi kuwa waadilifu.

"Hapa nimeelewa zaidi wajibu na majukumu yangu kama msimazi msaidizi wa uchaguzi na kwa uelewa huu ninaimani nitafanya vizuri na kufuata taratibu zote," alisema Paul Susu.

"Hapa nimeelewa vifaa ninavyo paswa  kuwa navyo kama msimamizi na inapaswa nitanye nini ninapokuwa katika kituo changu cha kazi," aliongeza Chenya Lugiko.

Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post