Na mwandishi wetu, Simiyu.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki ameupongeza Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutokana na huduma ambazo imekuwa ikitoa kwa
wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.
Waziri
Kairuki ametoa pongezi hizo (leo Agosti 3, 2020) wakati alipotembelea
katika banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa
katika viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Waziri
Kairuki alitoa pongezi hizo baada ya kupata maelezo ya shughuli za Mfuko yaliyokuwa
yakitolewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence ambapo
Waziri alivutiwa na majibu ya namna fidia inavyolipwa kwa mfanyakazi aliyeumia
au kufariki kutokana na kazi.
“Mwisho
wa siku mtu amepata ulemavu wa kudumu angalau consolation (faraja) anayopata ni kuona wanae wanaendelea vizuri au
kama amefariki walau fidia isaidie watoto na mjane pia, lengo la serikali ni
ku- support for real, ninawapongeza
sana kwa kazi nzuri mnayofanya.” Alisema Waziri Kairuki ambaye alikuwa amefuatana
na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga.
Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi unashiriki katika maonesho hayo ili kukutana na wadau wote na wananchi kwa ujumla wakiwemo wafanyakazi kutoka sekta ya Umma na Binafsi
Kauli
mbiu ya mwaka huu ya maonesho hayo yanayofanyika mkoani Simiyu kwa mwaka wa
tatu mfululizo ni “Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora
2020.”.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia uwekezaji Angellah Kairuki (wapili kushoto), akifuatana na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (wa kwanza kushoto), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwenye viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu jana. Wapili Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence akiwa na Afisa kutoka ofisi ya utawala Neema Mushi.
Afisa kutoka ofisi ya utawala WCF, Neema Mushi.
Wananchi wakipata maelezo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi kwenye banda la WCF viwanja vya Nyakabindi.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence (kulia), akimfafanulia jambo mfanyakazi huyu aliyetembelea banda la WCF viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu Agosti 3, 2020.
Social Plugin