Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoka kukagua
mzani wa Nangurukuru uliopo mkoani Lindi wakati alipowasili mkoani humo kwa
ajili ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli baada ya kukagua
barabara ya kutokea Lindi hadi Dar es Salaam na kutoridhishwa na hali ya
miundombinu ya barabara hiyo.
Naibu
waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga, kuhusu
ukarabati wa sehemu iliyoharibiwa na malori ya mizigo ya mawe katika barabara
ya Mtwara - Lindi - Dar es Salaam.
Viongozi
na Wataalam kutoka wizara ya Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
wakisikiliza maelezo kutoka kwa wasafirishaji wa mawe katika eneo la
Kilanjelanje mkoani Lindi tayari kwaajili ya kusafirishwa kuelekea jijini Dar
es Salaam.
Muonekano
wa sehemu ya barabara iliyoharibika kutokana usafirishaji wa mizigo kwa wingi
baada ya ongezeko kubwa la magari ya mizigo yanayotumia barabara hiyo ya Lindi
– Dar es Salaam na kupelekea kuharibu miundombinu ya barabara hiyo.
Lori
la mizigo likipakia mawe katika eneo la Kilanjelanje mkoani Lindi tayari
kwaajili ya kusafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ametengua nafasi
ya Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Pwani na Lindi
kutokana na kutoridhishwa na usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi ya barabara
ya Dar es Salaam - Kilwa - Lindi hadi Mingoyo yenye urefu takriban kilometa
450.
Aidha,
ameagiza Mameneja wapya wa mikoa hiyo na mameneja wa mikoa mingine kuhakikisha
wanaziba mashimo yote yaliyopo kwenye barabara zao ndani ya saa 48 kuanzia muda
wa shimo hilo linapojitokeza.
Mhandisi
Kamwelwe, ametoa agizo hilo akiwa mkoani Lindi ikiwa ni utekelezaji wa
agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
baada ya kutoridhishwa na hali ya miundombinu ya barabara kuanzia Nangurukuru
hadi Mbwemkuru wakati alipoikagua barabara hiyo siku chache zilizopita ambapo
pamoja na mambo mengine amesema kuwa hadi sasa bilioni 10 zimeshatengwa kwa
ajili ya zoezi la kuziba mashimo yote kabla hayajaleta athari zingine.
"Nimetengua
nafasi za watendaji hawa wawili kwa makosa yaliyojitokeza katika barabara hizi
zinazounganisha mkoa kwa mkoa na hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu
nahitaji wananchi wawe wanapita salama katika barabara hii", amesema
Waziri Kamwelwe.
Waziri
huyo ameeleza kuwa sehemu kubwa ya barabara iliyoathirika ni kuanzia eneo la Muhoro
mkoani Pwani hadi Mbwemkuru mkoani Lindi yenye jumla ya urefu wa kilometa
190 na zote zipo katika utaratibu wa kuanza kukarabatiwa.
Waziri
Kamwelwe amebainisha kuwa ataendelea kusimamia muongozo wake alioutoa mwezi
Juni mwaka huu kuwa barabara yoyote yenye mashimo katika barabara kuu na za
mikoa basi huyo Mhandisi wa Mkoa ajiondoe mapema kwani hayuko tayari kufanya
kazi na wataalamu wasio weledi na kushindwa kusimamia rasilimali fedha na watu
vizuri.
Ameongeza
kuwa hadi sasa Serikali imeshatoa kiasi cha fedha bilioni 40 kwa ajili ya
matengenezo ya barabara zote nchini zilizoathriwa na maji ya mvua.
"Fedha
zipo sasa sitarajii kuona barabara yoyote hapa nchini ina mashimo, huyo Meneja
ambaye barabara zake zina mashimo tutamalizana hapo hapo", amesisitiza
Mhandisi Kamwelwe.
Waziri
Kamwelwe ameelezea umuhimu wa barabara hiyo kiuchumi ambayo ilijengwa
toka mwaka 2008 na kusema kuwa ongezeko la usafiri wa abiria na
usafirishaji wa bidhaa, mazao na malighafi za viwandani katika kipindi cha
miaka hii 12 ndiyo imetuonesha namna ya kujipanga upya katika ukarabati wa
barabara hii.
"Tunaleta
watalaamu katika barabara hii kwa ajili ya kuanza kusanifu upya na kuona
kwanini imeharibika kabla ya wakati wake na maandalizi yanaendelea
vizuri", amefafanua Waziri Kamwelwe.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akiongozana na Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Arch. Elius Mwakalinga, wameikagua pia sehemu ya barabara
hiyo na kueleza kuwa hatua za awali za ukarabati zimeanza ambapo
kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, mwaka huu.
Naibu
Waziri Kwandikwa amewataka wakandarasi watakaopewa kazi ya ukarabati wa
barabara hiyo kukamilisha kabla ya kuanza kwa mvua za vuli zinazotarajiwa
kunyesha hivi karibuni kwani barabara hiyo ina mchango mkubwa sana wa kiuchumi
na kijamii kwa wakazi wa Nyanda za Kusini.
Naye,
Katibu Mkuu Arch. Elius Mwakalinga, amewahakikisha wakazi wa mikoa ya Pwani,
Lindi na Mtwara kuwa maeneo ya barabara yaliyokuwa yameharibika yameanza
kufanyiwa matengenezo kwa sababu asilimia 80 ya bajeti ya wizara imetengwa kwa
ajili ya ukarabati wa barabara nchini.
“Sina
mashaka na kazi ya ukarabati wa sehemu ya barabara hii kwa sababu fedha
zipo na mimi nipo eneo la tukio tangu Rais Magufuli alipotoa agizo la
ukarabati wa barabara hiyo na hadi sasa maandalizi yanaendelea vizuri",
alisisitiza Arch. Mwakalinga.
Barabara
ya Dar es Salaam hadi Lindi inakarabatiwa kwa fedha za ndani na inatarajiwa
kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu hii ikiwa ni hatua zili
Social Plugin