Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikagua miundombinu ya Soko la
Samaki la Feri Jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya
ya Ilala, Charangwa Makwiro. PICHA NA MPIGA PICHA WETU
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameruhusu
matumizi ya jenereta kwa wavuvi wa ukanda wa Pwani wanaovua nyakati za
usiku hadi kufikia Januari 1, 2021 huku akitoa miezi miwili kwa Taasisi
ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kufanya mapitio ya utafiti huo
ili kujua chanzo na aina ya mwanga utakaouruhusiwa ambao hautaleta
athari kwenye ulinzi wa rasilimali
Pia
Waziri Mpina amegiza Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)
kufanya utafiti huo kwa kushirikiana na Wavuvi wa Soko la Feri ili
kupata matokeo ya pamoja ambayo hayatalalamikiwa na upande wowote huku
ukizingatia ulinzi rasilimali za uvuvi ili ziwe endelevu.
Akizungumza
na Wavuvi na Wafanyabishara wa Soko la Samaki Feri Jijini Dar es Salam
Waziri Mpina amesema katika kipindi hicho hadi kufikia Januari 1 mwakani
wavuvi wataruhusiwa kutumia jenereta na kwamba baada ya kukamilika kwa
utafiti huo Serikali itatoa uamuzi wa mwisho kuhusu suala hilo.
Hivyo
Waziri Mpina amewasihi wavuvi wote ukanda wa Pwani kuendelea kuiamini
Serikali yao ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli
kwani imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuhakikisha changamoto
zinazowakabili wavuvi zinaondoka na kwamba mambo yaliyokatazwa kisheria
ikiwemo uvuvi chini ya kina cha mita 50 pamoja na uvuvi wa dagaa wa
kutumia ringnet mchana ni lazima wavuvi wakaheshimu kwa manufaa ya
kizazi kijacho.
Waziri
Mpina amesisitiza kuwa kwa sasa kuvua kwa kutumia ringnet nyakati za
mchana ni uvuvi haramu hivyo Serikali haiwezi kuruhusu uvuvi wa aina
hiyo kwani tafiti zilizofanyika zimebaini kuwepo kuwa Uvuvi huo ni
hatari kwa ustawi wa mazalia ya viumbe wa baharini.
Waziri
Mpina alisema Serikali iko kazini na unafanyia kazi changamoto za
wavuvi huku akitolea mfano uboreshaji wa miundombinu ya soko la samaki
Feri ambapo kabla ya ziara yake kulikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu
wa vyoo bora ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilianza Ujenzi wa vyoo vya
kisasa matundu 16 huku Serikali ikijenga mabanda ya kupumzika wavuvi
kazi ambayo imefanyika na kuboresha mazingira ya soko hilo.
Waziri
Mpina alisema shabaha ya serikali ya awamu ya tano si kuwakwaza wavuvi
na si kukwamisha wavuvi kufanya shughuli zao bali ni kuwahimiza Wavuvi
kutumia zana bora za uvuvi zinazotakiwa na kusisitiza kuwa mvuvi
atakayekamatwa akivua kwa ringnet mchana atakamatwa kama mvuvi haramu
yoyote.
Katibu Tawala wa
Wilaya ya Ilala, Charangwa Makwilo aliishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kwa namna ilivyokaribu na wavuvi na kwamba kila kunapojitokeza
changamoto imekuwa ikifika kwa wakati sambamba na kushukuru kwa ujenzi
wa vyoo vipya vya kisasa matundu 16 yaliyojengwa na Wizara hali
iliyopunguza adha kubwa waliokuwa wanaipata wavuvi kwa kukosa huduma
bora za vyoo.
Pia
aliishukuru Wizara kwa kutenga Shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya
ukarabati wa miundombinu ya soko la Feri na kwamba itasaidia kuboresha
utoaji huduma tofauti na ilivyokuwa kabla ya uamuzi huo wa Wizara.
Kwa
upande wake Katibu wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Dar es Salaam, Feisal Ali
alimshukuru Waziri Mpina kwa uamuzi wa kuruhusu matumizi ya Jenereta
katika kipindi hiki cha mpito wakati wakisubiria kukamilka kwa tafiti ya
kujua chanzo cha mwanga kinachotakiwa huku wakishukuru kwa uamuzi wa
Serikali kuruhusu nyavu za milimita 8 kwa uvuvi wa dagaa.
Pia
alishukuru Serikali kwa uamuzi wa kuruhusu matumizi ya leseni moja kwa
uvuvi wa bahari ya Hindi kwani kwa kipindi kirefu wamekuwa
wakinyanyasika kwa kukamatwa wakitakiwa kuwa na leseni kwa kila
Halmashauri wanayokwenda kufanya shughuli za uvuvi.
Feisal
pia alishukuru Serikali kwa kupunguza mrabaha wa kusafirisha dagaa nje
ya nchi kutoka dola 1 mpaka Dola 0.16 kupitia Kanuni mpya ya Mwaka
2020 jambo lili ambalo limeleta manufaa makubwa kwenye sekta ya uvuvi na
kuongeza mapato ya wavuvi na wafanyabiashara wa mazao hayo.
Pia
Feisal kwa niaba ya Wavuvi wa Bahari ya Hindi alishukuru Serikali ya
Rais Magufuli kwa kupunguza leseni ya biashara ya kuuza mazao ya uvuvi
nje ya nchi kutoka Dola 2, 500 hadi Dola 250 kwa mwaka jambo ambalo
limeleta manufaa makubwa na kukuza uchumi huku wakishukuru kwa uamuzi
kubadilisha msimu wa uvuvi wa kambamiti hali inayowafanya kunufaika na
rasilimali hizo.
Social Plugin