WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati alipoongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Canon Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga
Canon Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga akizungumza wakati wa harambee hiyo |
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo |
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea mchango wa mtoto Nicolaus Galula wakati wa harambee hiyo
MENEJA wa Hotel ya Tanga Beach ya Jijini Tanga Joseph Ngoyo akizungumza jambo wakati wa harambee hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea mchango kutoka kwa Catherine Kitandula wakati wa harambee hiyo |
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka viongozi
wa dini kote nchini kuendelea kuliombea Taifa amani, umoja na mshikamano kuelekea
uchaguzi mkuu.
Ummy
aliyasema hayo leo wakati alipoongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la
Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo Chumbageni
Tanga.
Katika
harambee hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na
viongozi wa dini wakiwemo waumini huku kwaya mbalimbali zikitumbuikiza.
“Lakini
pia tunawashukuru viongozi wa dini kwa jinsi walivyotuunga mkono kwa sala za
kila siku katika mapambano dhidi ya Corona na mungu akatuepusha na janga hili
hivyo niwaombe hata wakati huu nchi ikielekea kwenye uchaguzi mkuu tuendelee
kuiombea nchi”Alisema Waziri Ummy,
“Nimekuwa
nikipata ujumbe kutoka kwa mawaziri wa nchi nyengine Afrika tumefanya kitu gani
mpaka hakuna Corona nisema kwamba ugonjwa huo umetoweka kutokana na Mungu ameipenda Tanzania”.
Awali
akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu wa Kanisa hilo Cyprian Mtweve alisema
lengo la harambee ya leo katika kuadhimisha sikukuu ya Mt.Agustino wa Hippo ni
kupata kiasi cha sh.milioni 125 kwa ajili ya kuezeka kanisa.
Alisema
wanaamini kiasi hicho sio kikubwa kwa Mungu cha kushindwa kupatikana huku
wakimshukuru mgeni rasmi kuwaongozea zoezi la harambee hiyo na kushiriki kwa
moyo na kwa ukamilifu.
Aidha
alisema upanuzi wa jengo la kanisa hilo umekuwa ukifanywa kwa kulirefusha kwa
kiwango ambacho mawasiliano baina ya kasisi anayeongoza ibada madhabahuni na
waumini wanaokaa viti vya mwishoni nyuma ya kanisa yanakuwa hafifu kwa sababu ya
umbali.
“Jengo
hili limejengwa kwa kutumia teknologia ya zamani isiyohimili uwekwaji wa mifumo
mbalimbali ya kisasa ikiwemo ile itakayoboresha ibada”,alisema.
Miongoni
mwa viongozi ambao wamechangia kwenye harambee hiyo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi na Profesa Palamagamba Kabudi wakiwemo wakuu wa wilaya .