MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA MAZINGIRA DUNIANI : SHINYANGA WAASWA KUENDELEA KUJIKINGA NA MAGONJWA YANAYOSABABISHWA NA UCHAFU

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Neema Simba mkoa wa Shinyanga amewataka wananchi mkoa wa Shinyanga kuendelea kujikinga na magonjwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira na kujenga vyoo ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza.

Neema Simba ameyasema hayo leo Jumamosi Septemba 26,2020 ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mazingira Duniani ambapo Kauli mbiu ya kidunia mwaka 2020 ni ‘Environmental health is akey of public health intervention in diseases pandemic prevention’ na Kauli mbiu ya kitaifa ni ‘Epuka magonjwa ya mlipuko kwa kudumisha uchukuaji wa tahadhari za kujikinga na athari za kiafya zinazoweza kutokana na mazingira’

"Tunapoadhimisha siku ya afya ya mazingira duniani tunawaasa wananchi
wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kujikinga na magonjwa
yanayosababishwa na uchafu wa mazingira , kama vile kauli mbiu
yetu ya mwaka huu  2020 inavyosema “Epuka
magonjwa ya mlipuko kwa kudumisha uchukuaji wa
tahadhari za kujikinga na athari za kiafya zinazoweza
kutokana na mazingira”, amesema Neema

"Kuna mbinu mbalimbali zinazotumika kuhamasisha wananchi
kama vile ujenzi wa vyoo bora, uwekaji wa vifaa vya kunawa
mikono, utunzaji wa vyombo baada ya kuoshwa, utupaji wa taka
ikiwemo uwekaji wa chombo cha kutupia taka au shimo la kutupia
taka, hivi vyote vinatekelezeka katika Mkoa wetu wa Shinyanga",ameongeza 


Akitoa taarifa ya vyoo mpaka Juni, 2020 katika mkoa wa Shinyanga,amesema kaya zenye vyoo bora  zipo 60%, kaya zenye vyoo aina zote – 98%, kaya zisizo na vyoo 2% na kaya zenye vyombo vya kunawia mikono – 32.38%, kaya zenye vyoo vya asili  38% na kaya zinazotunza vyoo kwa kuvifanyia usafi ni  26.54%.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post