Mgombea ubunge Jimbo la Bukoba Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wakili Stephen Byabato
Na Ashura Jumapili, Bukoba
Ombi hilo limeombwa na Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukoba mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Wakili Stephen Byabato wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa chama hicho mkoani Kagera.
Wakili Byabato, alisema Jimbo la Bukoba Mjini halikuwa na mtandao hapakuwepo na mtu wa kupokea simu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
Alisema Rais Magufuli,amefanya mambo mengi mazuri katika maeneo mbalimbali lakini Bukoba hapakuwa na Mnara wa mawasiliano kwa maana ya mbunge anayetokana na CCM hivyo alikuwa anafanya kazi katika mazingira magumu.
Alisema Mnara wa Bukoba unaotakiwa kujengwa ili kuunganisha mawasiliano kati ya Rais na wananchi ni kumchagua yeye kwa kumpigia Kura za kutosha Oktoba 28 mwaka siku ya uchaguzi mkuu.
"Wananchi Mnara unaotakiwa kujengwa hapa Bukoba mjini ni Mimi Wakili Stephen Byabato ninayetokana na chama Cha mapinduzi kwa kunichagua kwa kura za kishindo pamoja na Rais wetu Dk. John Magufuli katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu hivyo tunaomba Kura nyingi za kutosha",alisema Wakili Byabato.
Alisema maendeleo Bukoba mjini yapo lakini hayatoshelezi maana hapakuwepo na mtu wa kufanya naye kazi mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti alijitahidi sana hakuwa na msaidizi.
"Tunahitaji kujenga Mnara Bukoba mjini ili mawasiliano yapatikane kwa urahisi na maendeleo yafike kwa wakati na wananchi wafaidike na matunda ya uongozi Bora",aliongeza Wakili Byabato.
Alisema Jimbo hilo halikuwa na mwakilishi wa wananchi wa muda wa miaka mitano Sasa umefika wakati wa wananchi kufanya chaguo lililo sahihi kwa kunichagua Chama Cha Mapinduzi.
Uzinduzi huo pia ulipambwa na burudani kutoka kwa Isha Mashauzi mwimbaji wa taarabu.
Jimbo hilo la Bukoba lilikuwa upinzani tangu mwaka 2015 Wilfred Rwakatare aliposhinda kuwa mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mgombea ubunge Jimbo la Bukoba Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wakili Stephen Byabato
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo