Na Helena Magabe
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Esther Matiko ameshukuru kupungua kwa mfumo dume Tarime.
Akizungumza katika uzinduzi wake wa kampeni jana uliodhuriwa na maelfu ya wananchi, Esther Matiko aliwashukuru Wananchi kumchagua kipindi kilichopita kuwa Mbunge wao.
"Mlivunja miiko kuwa Mwanamke hawezi,Tarime haiwezi kuongozwa na Mwanamke lakini iliwezekana mkanichagua",alisema Esther Matiko.
Alisema kama ni maendeleo amefanya mengi yanaonekana amejenga shule mpya 8,amekakarabati chuo cha ufundi FDC pamoja na chuo cha ulimu TTC.
Aidha aliwaomba wananchi wampe ridhaa ya kuendelea kuwatumikia miaka mitano ijayo.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya alimwombea kura Esther Matiko kwa kuwa anawaza maendeleo tu.
" Siasa za Chadema ni hoja si Vioja, wanaotukana acha watukane tu Esther Matiko anawaza maendeleo tu", alisema Bulaya
Naye Mgombea Ubunge Jimbo la Serengeti Catherine Nyankao Ruge aliwaomba Wananchi wamuongeze Esther Matiko miaka mingine mitano ili aendelee kuleta maendeleo Tarime.
Alisema Esther Matiko pamoja na Esther Bulaya ndiyo wamemnoa na kumpa ujasiri mpaka kufikia hapo alipo na kuamua kugombea na kwamba wanawake hao wamekuwa mfano wa kuigwa.
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini John Heche alisema Tarime hawataki Mwakilishi wa Serikali bali wa Wananchi.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara Lucas Ngoto alisema chama chao kina akili ya kubuni miradi.
Alisema chama chao kimebuni miradi mingi kwa muda miaka mitano kwa kutumia fedha za vyanzo vya ndani pekee.
Social Plugin