Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha : KATAMBI AKIMWAGA SERA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI CCM NDEMBEZI.... 'MIMI NI MTU WA KAZI'

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi Oktoba 28,2020 kumchagua kuwa mbunge kwani amedhamiria kufanya kazi kuwatumikia wananchi.

Katambi ameyasema hayo leo Ijumaa Septemba 25,2020 kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mabambasi kata ya Ndembezi ambao umehudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM waliojitokeza kusikiliza sera za Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi mkuu 2020.

“Ndugu zangu niliamua kuachana na kazi ya Ukuu wa wilaya ya Dodoma na kuamua kuja hapa Shinyanga mjini kugombea ubunge. Ukiona kuku kwa mganga wa kienyeji ujue ameponzwa na rangi yake, basi na mimi nimeponzwa na nyinyi ndiyo maana nipo hapa. Naombeni kura ndugu zangu. Mimi ni mtu wa kazi,nitawatumikia kwa moyo wangu wote,kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.Tutabanana hapa hapa sitaondoka”,amesema Katambi.

Katambi amesema atahakikisha anapigania maslahi ya wakulima na wafugaji na kuboresha sekta ya afya kwa kujenga zahanati na vituo vya afya, elimu kwa kujenga vyoo,maabara na madarasa na ujenzi wa barabara akisisitiza kuwa anataka kila mtaa uwe na barabara za kiwango cha lami.

Akinadi sera za CCM, Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi, David Nkulila amewaomba wananchi wamchague tena kuwa diwani wa kata hiyo ili kuendeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Nkulila amesema ataendelea kutatua kero za wananchi ikiwemo za ardhi,afya,barabara na kuhakikisha anasimamia mapato ya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulam amewaomba wananchi wa Ndembezi kumchagua David Nkulila kuwa diwani wa kata hiyo akidai kuwa Nkulila ni mtu mwenye msimamo na amekuwa mtetezi wa wanyonge na kupigania maslahi ya wananchi huku akiwaomba wamchague Katambi kuwa Mbunge kutokana na kwamba ni mtu wa kazi asiyependa porojo.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akizungumza katika mkutano wa Kampeni leo Ijumaa Septemba 25,2020 katika uwanja wa Mabambasi kata ya Ndembezi ambapo amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi Oktoba 28,2020 kumchagua kuwa mbunge kwani amedhamiria kufanya kazi kuwatumikia wananchi. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi katika kata ya Ndembezi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Ndembezi katika mkutano wa Kampeni leo Ijumaa Septemba 25,2020 katika uwanja wa Mabambasi kata ya Ndembezi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulam
Wananchi na wanachama wa CCM wakimsikiliza Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi 
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Ndembezi katika mkutano wa Kampeni leo Ijumaa Septemba 25,2020 katika uwanja wa Mabambasi kata ya Ndembezi. 
Wananchi na makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi CCM.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Ndembezi katika mkutano wa Kampeni leo Ijumaa Septemba 25,2020 katika uwanja wa Mabambasi kata ya Ndembezi. 
Msanii Nyassani akitoa burudani kwenye mkutano wa Kampeni za Uchaguzi CCM katika kata ya Ndembezi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi  akishikana mkono na Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi, David Nkulila wakati Msanii Nyassani (aliyevaa nguo ya njao) akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi CCM kata ya Ndembezi
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi  akifurahia na wananchi wakati Msanii Nyassani (aliyevaa nguo ya njano kushoto) akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi CCM kata ya Ndembezi
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akifurahia na wananchi wakati Msanii Nyasani (kushoto) akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi CCM kata ya Ndembezi
Msanii Nyassani akicheza muziki na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi, Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila na viongozi mbalimbali wa CCM kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi CCM kata ya Ndembezi
 Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulam akiwaombea kura wagombea wa CCM akiwemo Mgombea Urais Dk. John Pombe Magufuli, mgombea Ubunge Patrobas Katambi na Mgombea udiwani kata ya Ndembezi David Nkulila

Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi David Nkulila akionesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati akiomba kura kwa wananchi wa Ndembezi wamchague kuwa diwani wa kata hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulam 
Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi David Nkulila akiomba kura kwa wananchi wa Ndembezi wamchague kuwa diwani wa kata hiyo.
Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi David Nkulila akiomba kura kwa wananchi wa Ndembezi wamchague kuwa diwani wa kata hiyo.
Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi David Nkulila akinadi sera za CCM na kueleza mafanikio makubwa katika kata hiyo yanayotokana na CCM
Mgombea Udiwani Viti Maalumu Zuhura Waziri akiwaombea kura wagombea wa CCM.
Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Grace Bashemu na wagombea udiwani viti maalumu wakiwa wamepiga magoti wakiwaombea kura wagombea wa CCM akiwemo Mgombea Rais  Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea Ubunge Patrobas Katambi na mgombea Udiwani David Nkulila
Lydia Lefi aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA na kuhamia CCM akiwaombea kura wagombea wa CCM
Makada wa CCM wakifurahia jambo kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com