Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemhukumu Mzee wa miaka 84,Ally Baruhani Macho miaka 4 jela kwa kosa la kugushi hati ya kiwanja.
Hukumu hiyo imetolewa hii leo Septemba 21,2020 na Hakimu Mkazi Rashidi Chaungu ambapo upande wa jamhuri ulikuwa na jumla ya mashahidi wa 5 na upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi 4.
Hakimu Chaungu amesema kuwa ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri dhidi ya Mshtakiwa, Ally Baruhani Macho.
Aidha Upande wa Jamhuri uliowakilishwa na Mawakili Ashura Mzava na Kija Elias umeeka nia ya kukataa rufaa dhidi ya adhabu hiyo iliyotolewa kwa Mshitakiwa.
Mshtakiwa Ally Baruhani Macho anadaiwa kutenda kosa la kugushi na kuwasilisha Nyaraka za uongo ambapo aligushi hati ya kiwanja Plot namba 894 block G kilichopo Tegeta Jijini Dar es salaam Mali ya Haidari Kavira.
CHANZO - EATV
Social Plugin