Mkuu wa wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es salaam Ng'wilabuzu Ludigija leo Septemba 1,2020 amefanya ziara katika kata ya Chanika mtaa wa Yonge kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Ludigija amewatoa hofu wananchi wa Chanika na kuwahakikishia kuwa watapata umeme majumbani na kwamba serikali itaendelea kutatua kero ya maji na barabara.
Hata hivyo wananchi wamefurahia kuletewa mrejesho wa kila serikali inayotarajia kufanya katika mitaa yao na wameahidi kujitokeza katika zoezi la kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28,2020
Mkuu wa wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es salaam Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza na wananchi katika kata ya Chanika mtaa wa Yonge kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.
Social Plugin