Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : CHADEMA WAZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO SHINYANGA MJINI…SALOME MAKAMBA AZUA GUMZO AKIFANYIWA TAMBIKO LIVE JUKWAANI MAELFU WAKISHUHUDIA

Mzee wa kimila akimfanyia tambiko maalumu Jukwani Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini leo eneo la Ngokolo 
**
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Maelfu ya wakazi wa Shinyanga Mjini wamejitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi za Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Uzinduzi huo wa aina yake ulioambatana tukio la Mgombea huyo wa Ubunge Salome Makamba ‘Ng’wana O – Shimba’ kufanyiwa tambiko  maalumu na kupewa silaha za jadi na wazee wa kimila umefanyika leo Jumanne Septemba 8,2020 katika eneo la Ngokolo Mitumbani Mjini Shinyanga.

Shangwe zilisikika zaidi mara baada ya Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Salome Makamba kumaliza mkutano wake wa hadhara ambapo viongozi wa CHADEMA waliwakaribisha Jukwaani wazee wawili wa Kisukuma wakiwa na vifaa vya kimila ambapo mmoja wa wazee hao alizua gumzo akimfanyia tambiko Mgombea Ubunge Salome Makamba Mubashara 'Live' Jukwaani. 

Akinadi sera zake, Salome Makamba ambaye ni Mwanasheria amewaomba wakazi wa Shinyanga kutofanya makosa katika uchaguzi Mkuu 2020 hivyo wamchague yeye kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwani amedhamiria kuwaletea maendeleo wananchi.

Makamba ambaye ni mwanamke pekee kati ya wagombea saba wanaowania ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini, pamoja na mambo mengine ya kuwaletea maendeleo wananchi, amesema miongoni mwa vipaumbele vyake ni masuala ya elimu,afya uchumi huku akiahidi kuibeba ajenda ya kukomesha suala la ndoa na mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga na kupigania watoto wa kike wanaopata ujauzito kuruhusiwa kuendelea na masomo.

Amesema akifanikiwa kuingia bungeni atahakikisha wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini wananufaika na rasilimali zilizopo mkoani Shinyanga ikiwemo madini na mifugo ili kuondokana na umaskini. 

Naye Meneja Kampeni wa Salome Makamba, Juma Protas alisema uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 siyo wa kufanya masihara na kuwasihi wananchi kuacha ushabiki wa siasa hivyo wafanye maamuzi sahihi kwa kuchagua wagombea wa CHADEMA akiwemo Tundu Lissu kuwa Rais wa Tanzania,wabunge na madiwani wa CHADEMA ili kuwaletea maendeleo wananchi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwasalimia wananchi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni  katika eneo la Ngokolo leo Jumanne Septemba 8,2020. Kulia ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi ambaye ni Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiomba kura kwa wananchi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni  katika eneo la Ngokolo leo Jumanne Septemba 8,2020

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni  katika eneo la Ngokolo leo Jumanne Septemba 8,2020

Meneja Kampeni  wa Salome Makamba, Juma Protas (kushoto) Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwa jukwani.
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo
Vijana wa Sarakasi wakionesha vipaji vyao
Vijana wa Sarakasi wakionesha vipaji vyao
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA 
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA 
Mzee wa kimila akimvalisha vifaa/mavazi kimila Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati akimfanyia tambiko maalumu kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
Mzee wa kimila akimvalisha vifaa/mavazi kimila Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akifanyiwa tambiko maalumu kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
Wazee wa kimila wakiendelea kumfanyia tambiko Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Wazee wa kimila wakiendelea kumfanyia tambiko Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
 Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiendelea kufanyiwa tambiko maalumu kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
Wananchi wakifuatilia tukio la kufanyiwa tambiko
Wazee wa kimila wakiendelea kufanya tambiko
 Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa amesimama wakati  akifanyiwa tambiko maalumu kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
 Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiondoka eneo la mkutano wa kampeni baada ya kufanyiwa tambiko kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini

Wananchi wakichangia kampeni za CHADEMA wakati wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini

Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CHADEMA
Viongozi wa CHADEMA wakiwa wamekaa jukwaa kuu

Wananchi wakimsindikiza Salome Makamba baada ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA

Kada wa CHADEMA Joseph Kasambala ' kutoka timu ya Ushindi ya Salome Makamba' akiwaombea kura wagombea wa CHADEMA ( Salome Makamba - Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Emmanuel Ntobi - udiwani kata ya Ngokolo na Tundu Lissu - Urais Tanzania).

Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini, Hamis Ngunila akiwaombea kura wagombea wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu 2020.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com