Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akimvisha Medali Mshindi upande wa watoto aliyeshiriki mashindano hayo. Picha na Neema Sawaka
Mkurugenzi wa Shidepha+ Venance Mzuka akiongea na Washiriki wa mbio za Malaria Marathon.
Meneja wa T- Marc Hamid Al Alawy akiwahutubia washiriki wa mbio za Malaria Marathoni katika uwanja wa Halmashauri mjini Kahama.
***
Na Raymond Mihayo Kahama
Wananchi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi kila siku kwa ili kuufanya mwili kuwa na kinga imara na kuepukana na magonjwa hatari ambayo siyo ya kuambukiza.
Hayo yalisemwa jana Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee wakati akifunga mashindano ya riadha yenye lengo kuhamasisha kubadilisha tabia na kutokomeza Malaria (malaria Marathon) yaliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Comic Rerief la Uingereza kwa kushiana na Shirika la SHDEPHA+ Kahama.
"Ukifanya mazoezi kila siku ni rahisi kwa mwili kutumia kinga ya asili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kama vile Shikizo la Moyo, Kisukari na Mgonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza kwa binadamu",alisema Dkt. Mzee.
Dkt. Mzee alisema kuwa mbio hizo zimeambatana na ujumbe wa kutokomeza Malaria Mkoa wa Shinyanga huku zikiwashirikisha wakimbiaji kutoka Wilaya ya Kahama na nje ya Kahama yaani Mkoani Manyara na Arusha wa jinsi ya kike na Kiume huku wakikimbia umbali wa kilometa 21.
Kwa upande wake Afisa Michezo kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama Lupola Mkomwa alisema kuwa lengo la mbio hizo ni kutokomeza ugonjwa wa Malaria katika Halmashauri sita zilipo katika Mkoa wa Shinyanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SHDEPHA+ Tanzania Venance Mzuka alisema kuwa shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria na kuhimiza michezo na maagizo mbalimbali yanayotolewa na Serikali.
Alisema kuwa njia mojawapo iliyotumika katika kutokomeza ugonjwa huo ni pamoja na kutumia mashindano kama hayo ngoma za asili kutoa elimu kwa jamii iliyopo maeneo yenye maambukizo makubwa vijijini hali ambayo imechangia kuleta mabadiliko chanya kwa ugonjwa kupungua kiasi kikubwa.
Mbio hizo za Malaria Marathon zilimalizika huku washindi kwa upande wa Wanaume akiwa ni Elisante Elibariki aliyemaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa dakika 43, mshindi wa pili alikuwa ni Halipha Atanas aliyetumia muda wa dakika 44.28 huku mshindi wa tatu akiwa Adam Neta akitumia dakika 45 kumaliza mbio hizo.
Kwa upande wa Wanawake aliyeongoza katika mbio hizo zlikuwa Hamida Nassoro aliyetumia dakika 49 huku aliyemfuata alikuwa Nyamizi Ngasa aliyetumia saa moja huku Esta Njingu aliyetumia saa 2.
Kwa upande wa watoto walioshiriki mbio hizo aliyeongoza alikuwa Seleman Salehe (16) Mwanafunzi wa shule ya sekondari Busoka, wa pili alikuwa Jeronimo Solomoni (10) na hivyo kutoa upinzani mkubwa kwa washiriki wengine wakubwa walioshiriki mbio hizo.
Mradi huo wa Malaria ambao ulikuwa wa miaka miwili utekelezaji wake umemalizika mwaka huu kwani ulianza mwaka 2018 huku Kauli mbiu wananchi kubadilisha tabia na kutokomeza Malaria ulifadhiliwa na Shirika la Comic Relief kutoka Nchini Uingereza kwa kushirikina na Shirika la SHDEPHA+ ambapo utekelezaji wake ulikuwa katika Halmashauri za Ushetu, Kahama Mji. Pamoja na Msalala zilizopo Wilayani Kahama pamoja na Halmashauri ya Kishapu, Shinyanga Mji pamoja na ile Shinyanga Vijijini.