Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi [CCM]Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde
Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewaomba wananchi kumpa kura ili aweze kuongoza tena kwa kipindi cha miaka mitano mingine kwani miaka mitano iliyokwisha alikuwa anajifunza .
Mavunde amesema hayo katika mkutano wa Kampeni uliokuwa unafanyika kata ya Ihumwa jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa endapo atachaguliwa kuwa kiongozi atafanya maajabu katika jimbo hilo.
“Nataka niwahakikishie DUWASA 2020/2021 wamepanga bajeti kuhakikisha maji yanasambaa katika eneo lote la kata ya Ihumwa,miaka mitano niliyokuwa naongoza nilikuwa najifunza vile”,amesema.
Aidha,Mavunde amesema atahakikisha wanakamilisha suala la barabara katika kata hiyo endapo atachaguliwa tena.
“Barabara Mhe.Rais aliahidi barabara tunahakikisha mkituchagua tena tunakamilisha ,pia umeme tutahakikisha unaenea maeneo yote 34 yaliyobaki”,amesema.
Social Plugin