Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Tarafa ya Makiungu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida jana.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akihubia kwenye mkutano huo.
Wananchi wa Tarafa ya Makiunga wakimsubiri Mtaturu.
Waendesha boda boda wakiongoza msafara wa mgombea huo.
Wananchi wa Tarafa ya Makiungu wakiwa na mabango yenye picha za mgombea Urais wa CCM wakati wa kumpokea Mtaturu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akionesha upendo kwa wapiga kura kwa kusalimiana nao.
Burudani ikiendelea katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Makiungu, Daud Kinjagahi, aakizungu kwenye mkutano huo.
Kada wa CCM, Gerald Mahami akizungumza kwenye mkutano huo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa, akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ikungi, Pius Sanka, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaj Juma Kilimba, akiwanadi wagombea udiwani wa Kata ya Makiungu, John Mathias (kulia) na Gabriel Dule (katikati) wa Kata ya Mngaa.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu amesema kutokukichagua chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu ni sawa na kupishana na gari la mshahara.
Mtaturu aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia Wananchi na wana CCM wa Tarafa ya Makiungu na Kata ya Mngaa katika mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni ndani ya jimbo hilo.
"CCM tumejipanga sawa sawa kwenye sekta zote hivyo kutokukichagua CCM ni sawa na kupishana na gari la mshahara." alisema Mtaturu.
Katika mkutano huo Mtaturu alikwenda mbali zaidi kwa kuwafananisha wagombea wengine wa nafasi ya Urais wa vyama vingine na mgombea Urais wa CCM kama ni kichuguu na Mlima Kilimanjaro au Mbingu na ardhi kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya mgombea wao.
"Hatuwezi kabisa kuwafananisha wagombea hao na Magufuli kwani amewaacha mbali sana." alisema Mtaturu.
Mtaturu alitumia nafasi hiyo kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kwa kipindi cha Miaka 5 ili aweze kufanya makubwa ndani ya jimbo hilo na pia alimuombea kura mgombea wao wa nafasi ya Urais Dkt John Magufuli,wabunge na madiwani wa chama hicho.
Alisema kugombea ubunge sio kujaza nafasi bali ni uwakilishi wa kuwatumikia Wananchi kwa kuwapelekea maendeleo na kuacha shughuli nyingine binafsi ambazo haziwahusu wananchi.
Aidha alisema kiongozi yeyote anapoaminiwa na wananchi kwa kupewa kazi ni lazima aache alama ya utendaji wake kama alivyofanya yeye katika maeneo mbalimbali alikoaminiwa kufanya kazi na kuhakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano kwa maendeleo katika majimbo yote Tanzania.
Akizungumzia ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 alisema ni kubwa kuliko ile ya 2015-2020 ambayo imebeba matumaini na kuwa na majibu ya kero za watanzania.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaj Juma Kilimba alisema uchaguzi wa mwaka huu ni wa muhimu hivyo wananchi wasifanye utani bali wamchague Rais ambaye atawafaa watanzania ambaye ni Dkt. John Pombe Magufuli.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa alisema wagombea pekee wanapaswa kuchaguliwa ni wale wanaotoka kwenye Chama hicho chenye sera na dira na sio kwa wagombea wengine ambao wamekuwa wakipitisha mabakuli kuomba wachangiwe.
Social Plugin