Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekanusha taarifa zinazoenea kwenye Mitando ya kijamii kuwa umesitisha utoaji wa baadhi ya dawa kwa watumiaji wahuduma hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma Septemba 5,2020 katika ofisi za Mfuko huo Mkurugenzi Mkuu Benard Konga amesema taarifa hizo zimeleta taharuki kwa wanachama wake
Amesema mfuko huo umejenga imani kubwa kwa wateja wake tangu kuasisiwa kwake mwaka 2001 kwa sasa una dawa 543 ambazo zikinyambulishwa zinafanya idadi ya dawa 975 baada ya kuongeza kitita cha mafao mwaka 2016
Amewatoa hofu wanachama wa NHIF hapa nchini na kuwataka kuendelea kutumia huduma hiyo na kutoa rai kwa wananchi kuepuka kutoa taarifa ambazo si sahihi.
Septemba 4 mwaka huu zilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mfuko wa taifa wa bima ya afya nchini(NHIF)umezifuta dawa 138 kutoka orodha ya dawa zinazotolewa na mfuko huo kwa wanachama wake.
Social Plugin