Muonekano eneo la tukio
Kijana Siraphop Masukarat mwenye umri wa miaka 18 kutoka Thailand amejikuta katika hali mbaya baada ya kuumwa nyeti zake na nyoka akiwa msalani.
Siraphop Masukarat alikuwa ameketi msalani/chooni huku akitazama video kwenye simu yake Jumanne, Septemba 8,2020 wakati alipohisi uchungu katika nyeti zake na kukimbizwa hospitalini ambapo madaktari walipendekeza ashonwe katika nyeti zake.
Akizingumza na Daily Mail, Siraphot alisema aligundua ameumwa na nyoka huyo baada ya kumuona akiinua kichwa chake.
"Nilikuwa najisaidia wakati ghafla nilianza kuhisi uchungu kwenye nyeti zangu. Ghafla nilimuona nyoka akiinua kichwa chake. Nilianza kutokwa na damu," alisimulia.
Aidha kidonda hicho kilitibiwa na dawa za antibiotic ili kuosha na kuua viini na sumu ya nyoka huyo.
Mamake aliwaarifu wataalam wa masuala ya wanyama waliowasili kwa haraka ili kuyaokoa misha ya kijana huyo aliyekuwa akihisi maumivu makali.
Social Plugin