Mwanaume ambaye ana umri wa miaka zaidi ya 80, alikuwa anakaribia kula chakula chake cha jioni wakati alipokasirishwa na kelele ya nzi aliyekuwa anamzunguka.
Aliamua kuchukua kifaa cha umeme kilichotengenezwa kwa ajili ya kuwaua mende akaanza kumuua nzi huyo lakini kwa bahati mbaya gesi ilikuwa inavuja katika nyumba iliyopo kando ya mto Dordogne nchini Ufaransa.
Gesi na kifaa chake vilisababisha mlipuko na sehemu ya paa la nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Parcoul-Chenaud ikaharibika.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo, mwanaume huyo ambaye hakuwa na silaha alibahatika kutoroka akiwa ameungua tu kwenye mkono wake.
Hata hivyo hatma ya nzi bado haijajulikana, chombo cha habari cha Sud-quest kilisema.
Mwanaume huyo kwa sasa amejihifadhi katika hoteli moja ya eneo hilo huku familia yake ikikarabati nyujmba yake.
Chanzo - BBC
Social Plugin