Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHINYANGA SUPER QUEENS YATEMBEZA KICHAPO CHA MBWA MWIZI KWA VIVA QUEENS

Timu ya Shinyanga Super Queens

Timu ya Shinyanga Super Queens imeendelea kuonyesha makali kwenye michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwa Soka la Wanawake, baada ya kucheza michezo mitatu mfululizo bila kufungwa.

Leo mapema asubuhi ya Septemba 2, 2020, Shinyanga Super Queens imetoa kipigo cha mbwa mwizi kwa wapinzani wao wa Viva Queens baada ya kuishushia mvua ya mabao kwa kuikung'uta magoli 16-0 na kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Katika michuano hiyo inayofanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya Puma na Fountain Gate, Shinyanga Super Queens ambayo inasaka nafasi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao ilianza kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mkwawa Queens.

Katika mchezo wa Pili kwenye kundi lao la C uliochezwa jana dhidi ya Mt. Hanang ya Manyara, Vijana wa Shinyanga walilazimishwa sare ya mabao 3-3.

CHANZO : Shinyanga Press Club Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com