Mtendaji Mpya wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez
Mtendaji Mpya wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez
Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam, imemtangaza Barbara Gonzalez kuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo akitwaa nafasi iliyoachwa na Senzo Mazingisa mwezi mmoja uliopita.
Mwanadada huyo ambaye ameshafanya kazi katika taasisi mbali mbali ndani na nje ya nchi ya Tanzania amethibitishwa leo kufuatia kikao cha bodi ya wakurugenzi kufikia makubaliano ya pamoja.
Baada ya Senzo Mazingisa kutimkia kwa wa watani wao wa jadi timu ya Yanga, Simba wamekuja na jibu la swali ambalo lilitawala vichwani mwa wapenda michezo Tanzania kuhusiana na nani angeajiriwa kuziba nafasi hiyo ndani ya Simba.
Mpya wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez, amesema anatarajia makubwa ndani ya klabu hiyo kubwa likiwa kubeba mataji yote waliyopata msimu uliopita.
Akizungumza mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari na Mwenyekiti wa bodi ya Simba Mohammed Dewji, Gonzalez alisema kuwa kutokana na uzoefu aliokuwa nao ndani ya klabu ya Simba ana matumaini ya kufanya makubwa.
Alisema mara baada ya kupewa nafasi ya kukaimu akiweza kujifunza mengi, hivyo hana ugeni wa utendaji.
"Nina ahidi makubwa simba, ikiwa ni pamoja ya kutetea makombe yote tuliyochukuwa msimu uliopita, kikubwa ushirikiano wa wanachama, mashabiki na wadau wote wa Simba kwa ujumla" alisema Gonzalez.
WASIFU WA BARBARA GONZALEZ.
-Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji (Mo Dewji Foundation)
-2016:Mwezi wa Aprili, Alijiunga na taasisi ya Mo Dewji inayojishughulisha na maendeleo ya jamii ya Watanzania kupitia Afya na Elimu.
-Mshauri Mkuu (Conceltant): Kampuni ya Deloitte kwa miaka miwili.
-Mshauri (Consultant) Shirika la VSO, London.
-Kazi kwa kujitolea, (Interm): Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kupambana na kuzuia uhalifu, pia makazi na lile la Wanawake (UNDOC,UN-Women na UN-Habitat).
ELIMU YA BARBARA GONZALEZ.
Masters,MA:Development
-Chuo :London School of Economics and political Science, UINGEREZA.
-Bachelor Degree , BA: Economics and political Science
-Chuo: Manhattan Ville College
New York, MAREKANI.
UZOEFU NDANI YA SIMBA:
-Amefanya kazi za kuelekea kwenye mabadiliko ya kimfumo ndani ya Simba.
-Amefanya kazi za utendaji (CEO) akikaimu nafasi ya Senzo Mazingiza aliyetimkia Yanga kwa mwezi mmoja.
Social Plugin