Droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Soka Trivia’ imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkaazi wa Zanzibar, Ally Bangeni Haji amejishindia 10m/-.Haji akiongea baada ya kupigiwa simu na Mtaalam wa Huduma za Ziada kutoka Tigo, Fabian Felician, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema anayo furaha kufanikiwa kuibuka mshindi katika promosheni hiyo.
“Sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, naishukuru familia yangu na Tigo, familia yangu imenisaidia pakubwa kuweza kushiriki na hatimaye kuibuka mshindi, na Tigo kunipa fedha hizi,kwani mimi ni mkulima na fedha hizi zitanisaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto mbali mbali hapa nyumbani“alisema kwa furaha.
Mtaalam wa Huduma za Ziada kutoka Tigo, Fabian Felician, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja woteambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha taslimu ambazo zilitolewa na kampuni hiyo.
“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki tunachoelekea katika kuzindua msimu mpya wa promosheni ya Soka Trivia awamu ya nane, baada ya kumpata mshindi, leo tunamkabidhi mfano wa hundi wa 10m/-.
Tunawashukuru wateja wetu wote walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Agosti 2020”. alisema Felician.
Kwa kumalizia Felician aliwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinaendelea kubuniwa katika siku za usoni na kwa sasa ni rasmi Soka Trivia msimu wa nane umezinduliwa baada ya mshindi wa msimu wa saba kupatikana.
Mteja anaweza kutembelea www.tigosports.co.tz au atume SMS kwa kuandika neno SOKA kwenda 15670 au kupitia USSD *147*00# au *148*00# chagua SOKA.
Mteja atapokea SMS ya kumkaribisha ashiriki katika promosheni ya Soka Trivia msimu wa nane ,kila SMS utakayo jibu itatozwa 99TShs na kila jibu sahihi mteja atavuna pointi 100 na majibu ambayo sio sahihi atavuna point 25.
Zawadi za kushindaniwa ni Tshs 1,000,000 kila mwezi, Tshs 500,000 kila wiki, Tshs 50,000 kila siku. Na mshindi wa promosheni,ambae atakuwa na pointi nyingi zaidi atajinyakulia Tshs 12,000,000/-
Social Plugin