Katibu Mkuu Wizara ya viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akitoa neno la ufunguzi wa mdahalo huo kwenye ukumbi wa freedom Square Mazimbu Morogoro.
Washiriki wa mkutano huo kutoka Vyuo vikuu, Taasisi za Utafiti na Mashirika ya Kise rika ku na yasiyo ya Kiserikali kutoka mikoa mbalimbali nchini.Mkuu wa Mradi wa CREPEE Dkt. Faith Mabiki akizungumza kuhusu malengo ya Mradi na mdahalo huo wakati wa Ufunguzi wa mdahalo huo.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Maulid Mwatawala akizungumza kwa niaba ya Makamu mkuu wa chuo Prof. Raphael Chibunda wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo.
*************************************
Serikali inategemea matokeo ya Tafiti katika kufanya maamuzi na kusimamia maendeleo ya nchi ingawa mchango wa tafiti hizo katika kutunga sera na mipango ya maendeleo nchini sivyo ya kuridhisha.
Hayo ya yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe wakati akifungua Mdahalo wa wazi wa uchambuzi wa matokeo ya Tafiti katika utunzi wa sera na mipango ya maendeleo uliyofanya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Mkoani Morogoro.
Prof. Shemdoe amesema matokeo mengi ya Tafiti na taarifa za kitaalamu zinaishia kwenye majarida na makabati ya maktaba na ofisi wakati ukuaji wa uchumi unategemea Tafiti,Ubunifu na Uvumbuzi hivyo ni wazi kuwa serikali, vyuo vikuu/Watafiti na Wazalishaji ni vitu vitatu vinavyotegemeana.
“Serikali yetu imeazimia na kujitolea kuwezesha Taasisi mbalimbali na Mtafiti mmoja mmoja, kutafiti, kubuni,na kuboresha teknolojia katika sekta zote za Kiuchumi ikiwemo sekta ya viwanda ambayo kwa sasa inakuwa kwa kasi kubwa” Alibainisha Prof. Mdoe.
Katibu Mkuu huyo ametoa rai kwa watafiti wote nchini kuendelea kufanya Tafiti ambazo zitaibua ubunifu katika maendeleo ya sekta mbalimbali na hivyo mchango wao kupitia matokeo ya Tafiti kuchangia katika mipango ya maendeleo ya nchi.
Prof. Mdoe amewapongeza SUA kwa wazo hilo zuri kwa maendeleo ya nchi na kushukuru AIDEP na SUA kwa kifadhili mdahalo huu wenye lengo la kuanzisha Kituo cha Usanisi wa ushahidi wa Utafiti katika uundaji wa sera na mipango ya maendeleo nchini.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema Sera na Mipango ya kimaendeleo imekuwa inapungukiwa Urari katika Maendeleo ya Uchumi jamii na maendeleo endelevu.
Prof. Mwatawala amefafanua kuwa hiyo inatokana na ukweli kwamba wakati mwingine Tafiti na matokeo ya Tafiti zao hayatumiki ipasavyo kuakisi mahitaji halisi ya jamii na Taifa katika ujumla wake lakini pia wanaotunga sera na mipango ya maendeleo hawapati kirahisi na kwa lugha rafiki matokeo ya Tafiti ili kuyatumia katika utunzi wa sera.
Ameendelea kwa kusema kuwa ni wazi kuwa vyuo vikuu kote duniani ni joto I cha Taaluma na Tafiti na kwa muktadha huo SUA imeona ni vyema kutumia uwezo wake wa ndani na kwa kushirikiana na wadau wengine kuanzisha Kituo cha Usanisi wa matokeo ya Tafiti hapo SUA.
Malengo ya Kituo hicho amesema ni kisanisi ushahidi wa Utafiti katika uundaji wa sera na mipango ya maendeleo,kufanya mapitio ya machapisho ya Kisayansi na kuandaa kanzidata ya matokeo mbalimbali ya Tafiti,kuandaa mihutasari ya matokeo ya Utafiti katika lugha rahisi na kuandaa mihutasari ya sera.
“ SUA imekuwa na mchango Mkubwa sana kupitia Tafiti za kisayansi nchini na ulimwenguni kwa mfano kwa matokeo ya yaliyotolewa na Shirika la webomatrics Mwezi julai 2020, SUA umeshiba nafasi ya kwanza Kitaifa katika matumizi ya Tafiti zake (citation index) ambapo zaidi ya watafiti 82,220 duniani watumitumia machapisho ya SUA katika maandiko yao” Alisema Prof. Mwatawala.
Aliongeza “ Mchango huu ni Karibia mara mbili zaidi ya Chuo kilichoshika nafasi ya pili na ya tatu na ya nne kwa pamoja Kitaifa na nafasi SUA duniani imepanda kufikia nafasi ya 1161 kati ya vyuo vikuu Bora 5800 duniani”.
Prof. Mwatawala amesema pamoja na mafanikio hayo Kama Taifa bado tuma changamoto ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili kuchochea matumizi ya Tafiti, Sayansi,teknolojia na ubunifu Kama nyenzo ya maendeleo ya kiuchumi.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Mwatawala amesema ili kutatua changamoto hizo ni lazima Tafiti zifike ghala na kanzidata ya ofisi ya takwimu ya Taifa,zitumike katika utunzi wa Sera na mipango ya maendeleo ya Taifa,ziwafikie wadau wa maamuzi katika lugha rahisi na inayoeleweka na Pia ziwe na sehemu maalumu kuzichakata na kuzitafsiri na kuja na hoja mahususi katika Nyanja husika kwaajili ya mipango ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa mradi wa kujenga na kukuza uwezo wa Watafiti na watunga sera kuweza kusanisi matokeo ya Tafiti ili kuchangia kuleta maendeleo nchini CREPEERT Dkt. Faith Mabiki amesema Afrika ni bara lililo nyuma katika utoaji wa matokeo ya Tafiti licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu.
Ametolea mfano taarifa ya Shirika la elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ya Mwaka 2015 inaonesha bara la Afrika Linazalisha 2.6% tu ya matokeo ya Tafiti zote duniani lakini pia Afrika inachangia 2.9% ya watafiti wote duniani.
Dkt. Mabiki amesema kwa takwimu hizo ni kwamba uchangiaji wa Tafiti kwa maendeleo ya bara la Afrika na Tanzania ni mdogo na hivyo mradi wa CREPEE Ulizaliwa ili kuchangia katika Juhudi za Serikali kuongeza uwezo wa watafiti kusanisi matokeo ya Tafiti ili ziweze kutumika katika maamuzi mbalimbali ya kisera kwa maendeleo ya nchi.
Mkuu huyo wa mradi amesema ili kufikia lengo hilo Mradi unaendesha warsha za kujenga uwezo na uelewa wa namna Tafiti zinavyoweza kutumika katika kutoa mamauzi sahihi ya kisera pamoja na midahalo.